http://www.swahilihub.com/image/view/-/3887460/medRes/2050256/-/2m6vxk/-/kesa.jpg

 

Walimu 21,780 wako hatarini kupoteza kazi nchini Nigeria

Kalamu

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari Jangwani 

Na GEOFFREY ANENE na MASHIRIKA

Imepakiwa - Tuesday, November 14  2017 at  14:28

Kwa Muhtasari

Walimu 21,780 wako hatarini kupoteza kazi kwa kufeli mtihani ulioandaliwa na serikali ya Kaduna nchini Nigeria.

 

KADUNA, Nigeria

WALIMU 21,780 wako hatarini kupoteza kazi kwa kufeli mtihani ulioandaliwa na serikali ya Kaduna nchini Nigeria.

Gazeti la Vanguard linasema Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, anaunga mkono Gavana wa Kaduna, Nasir El-Rufai, kufuta walimu hao walioanguka mtihani wa umilisi wa kazi zao.

Rais Buhari alitangaza Novemba 13, 2017 kuunga mkono gavana huyo kuchukua hatua hiyo, huku Chama cha Nigeria Labour Congress (NLC) kikionya El-Rufai kujitayarisha kwa “maandamano makubwa kabisa” akipiga kalamu walimu hao.

Katika hotuba yake, gazeti hilo linasema, Rais Buhari alisikitishwa sana walimu kuanguka mtihani wa Shule za Msingi. Kulingana na Rais Buhari, hali ya elimu nchini Nigeria imezorota na inahitaji kutiliwa maanani sana. “Si siri kwamba kuna tatizo na ubora wa elimu yetu. Inahitaji kutiliwa maanani na kuimarishwa,” gazeti hilo limeripoti na kusema karibu watoto 13.2 milioni hawaendi shuleni katika taifa hili lililo na watu wengi barani Afrika (186 milioni).