http://www.swahilihub.com/image/view/-/4088558/medRes/1748129/-/p9llb5/-/don.jpg

 

Wanamuziki Don na Troy waaga dunia

Don Williams

Mwanamuziki marehemu Don Williams wa kutoka nchini Marekani. Picha/HISANI 

Na SAMMY WAWERU na MASHIRIKA

Imepakiwa - Saturday, September 9  2017 at  13:47

Kwa Mukhtasari

Taifa la Marekani na dunia kwa jumla inaomboleza kifo cha ghafla cha mwanamuziki tajika wa nyimbo za mtindo wa 'Country'.

 

TEXAS, Marekani

TAIFA la Marekani na dunia kwa jumla inaomboleza kifo cha ghafla cha mwanamuziki tajika wa nyimbo za mtindo wa 'Country'.

Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

"Williams ambaye ni mzaliwa wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi," afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza mapema Jumamosi.

Aidha Williams alianza kuimba kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971 na tangu wakati huo alichomoa vibao 17 zilizogonga ulingo wa sanaa ya muziki wa country side.

Nyimbo zake zilizovuma na kuongoa nyoyo za watu zaidi ni kama vile Gypsy Woman na Tulsa Time.

Mwanamuziki huyo alikuwa kielelezo cha wengi kama gwiji mnyenyekevu na mkwasi wa heshima.

Vibao vingine, hasa 'You're My Best Friend, I Believe in You, Lord na I Hope This Day Is Good pia vilikuwa miongoni mwa vilivyonoga duniani.

Wakati huo huo, nyota mwingine wa Country Music, Troy Gentry, imeripotiwa kwamba amekata kamba.

Troy alifariki Ijumaa katika ajali ya helikopta akiwa na umri wa miaka 50.

"Tunahuzunika kuthibitisha mwanamuziki mwingine wa Country Music Troy Gentry amefariki katika ajali ya helikopta iliyotokea mwendo wa saa saba mchana Medford, New Jersey," taarifa kwenye tovuti ya bendi hiyo ya wanamuziki wawili imesema.

Kufikia sasa chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.

Duru zaarifu wanamuziki hao walikuwa wameratibiwa kutumbuiza Medford Ijumaa jioni.

Mungu azilaze nyoyo zao pale mwenyewe anaona panafaa.