http://www.swahilihub.com/image/view/-/4567824/medRes/1976961/-/h6ipdoz/-/razak.jpg

 

Waziri Mkuu wa zamani Malaysia kushtakiwa

Najib Razak

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Bw Najib Razak, 64, asubiri kuswali Ijumaa, Mei 18, 2018, katika makao makuu ya chama cha Barisan Nasional Party (National Front) jijini Kuala Lumpur. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Friday, May 18  2018 at  10:14

Kwa Mukhtasari

  • Najib Razak huenda akafunguliwa kesi hivi karibuni
  • Waziri Mkuu mpya wa Malaysia Mahathir Mohamad asema ana uhakika waendesha mashtaka watajenga kesi hiyo kwa uzito kwa kuandaa mashtaka dhidi ya waziri mkuu huyo yanayohusiana na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika mfuko wa maendeleo uliofahamika kama “Malaysia Development Bhd”

 

KUALA LUMPUR, Malaysia

WAZIRI Mkuu aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa Malaysia wiki iliyopita Najib Razak huenda akafunguliwa kesi hivi karibuni, Waziri Mkuu mpya Mahathir Mohamad amesema.

Dkt Mahathir alisema ana uhakika waendesha mashtaka watajenga kesi hiyo kwa uzito kwa kuandaa mashtaka dhidi ya waziri mkuu huyo yanayohusiana na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika mfuko wa maendeleo uliofahamika kama “Malaysia Development Bhd”.

“Hivi sasa tunaendelea kushuka chini kabisa na maofisa waandamizi wengi wanajitolea kutoa taarifa, kwa vyovyote, wakiambatanisha na nyaraka.

“Tunafikiri katika kipindi kifupi kutakuwa na kesi dhidi yake, tutafungua mashtaka dhidi yake,” alisema na akaongeza kwamba alikuwa anakabiliwa na tatizo la “kujaribu kuwaamini watu wa kumchunguza.”

“Baadhi ya watu hawa ambao walikuwa naye walikuwa upande wake na hatumjui ni nani atakuwa mwaminifu kwa serikali hii.” (The Straits Times) usaidie kurejeshwa sehemu ya dola za Marekani 4.5 bilioni (RM18.19bil) zinazodaiwa kupotezwa na Kampuni ya 1MDB, Dk Mahathir alijibu tu: “Hakuna mpango”.

Dkt Mahathir aliamuru Najib azuiwe Jumamosi iliyopita asisafiri kuenda nje baada ya habari kuenea kuwa alikuwa anataka kuenda Jakarta, Indonesia kwa mapumziko mafupi.