http://www.swahilihub.com/image/view/-/4802428/medRes/2138201/-/7xcuwf/-/taric.jpg

 

Mpinzani afungwa maisha nchini Bangladesh

Kiongozi wa upinzani nchini Bangladesh, Tarique Rahman  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, October 12  2018 at  09:33

Kwa Muhtasari

Amepatikana na hatia ya uhalifu na kula njama ya mauaji

 

Dhaka, Bangladesh. Mahakama Kuu nchini Bangladesh imemhukumu kifungo cha maisha kiongozi wa upinzani Tarique Rahman, huku watu wengine 19 wakihukumiwa kifo kutokana na shambulizi la mabomu lililotokea mwaka 2004 dhidi ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina.

Mwendesha mashtaka, Mosharraf Hossain alisema kwamba wanamshukuru Mungu kwa hukumu hiyo.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kutangaza kwamba Tarique, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani anayeishi uhamishoni, amehukumiwa kifungo cha maisha.

Wote wamepatikana na hatia ya uhalifu na kula njama ya mauaji. Katika shambulio la 2004 kwenye mkutano wa hadhara wa Sheikh Hasina ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa upinzani na sasa ni Waziri Mkuu.

Watu 20 waliuawa katika shambulio hilo. Rahman alikimbilia mjini London 2008. Mama yake na Waziri Mkuu wa zamani Khalida Zia alihukumiwa kifungo cha miaka mitano Februari mwaka huo.