Mtoto za Zuma kizimbani kwa kesi ya mauaji na rushwa

Duduzame Zuma, mtoto wa Jacob Zuma ambaye alikuwa rais wa zamani wa Afrika Kusini  

Imepakiwa - Friday, July 13  2018 at  09:14

Kwa Muhtasari

Amekutwa na hatia ya kusabisha kifo iliyotokana na ajali ya gari

 

Johannesburg, Afrika Kusini. Duduzane Zuma, ambaye ni mtoto wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amekutwa na hatia ya kusabisha kifo iliyotokana na ajali ya gari iliyotokea mwaka 2014 wakati gari lake aina ya Porsche lilipomgonga basi mmoja na kusabisha kifo cha dereva wake.

Mwendesha mashtaka katika kesi hiyo, alisema mahakamani hapo kuwa mbali ya kifo cha Phumzile Dube pia ajali hiyo ilisababisha kifo kingine cha mwanamke mmoja ambaye alifariki dunia miezi mitatu baadaye. Ajali hiyo ilitokea eneo la of Sandton, Johannesburg.

Hata hivyo, mahakama haikuwa tayari kutaja adhabu itakayotolewa kwake lakini ilisisitiza itasomwa katika siku zijazo.

“Mahakama imeahirisha kusoma hukumu hadi hapo Agosti 23,” alisema msemaji wa Mamlaka ya Taifa ya Uendeshaji Mashataka (NPA), Phindi Mjonondwane.

Awali mahakama hiyo iliamua kutotoa adhabu dhidi yake kabla ya kubadili uamuzi wake. Mtoto huyo wa Zuma hakuwepo mahakamani wakati kesi hiyo ikisomwa.

Jumatatu iliyopita alifika katika mahakama nyingine akikabiliwa na mashtaka ya rushwa.