http://www.swahilihub.com/image/view/-/3241792/medRes/1348521/-/9xci6y/-/BDBUDGET0806KK%25282%2529.jpg

 

Korti yaombwa izuie Rotich kutoa pesa za kustawisha maeneo

Henry Rotich

Waziri wa Hazina Kuu Henry Rotich muda mfupi kabla ya kwenda Bungeni kusoma bajeti ya 2016/2017 Juni 8, 2016. Picha/SALATON NJAU 

Na RICHARD MUNGUTI

Imepakiwa - Tuesday, June 21  2016 at  23:18

Kwa Muhtasari

Mahakama Kuu Jumanne iliombwa imzuie Waziri wa Fedha Bw Henry Rotich asiipe Serikali pesa za matumizi na hazina ya kustawisha maendeleo katika maeneo bunge (CDF) kabla ya kurekebishwa kwa sheria mpya ya ustawi wa kitaifa-NCDF.

 

MAHAKAMA Kuu Jumanne iliombwa imzuie Waziri wa Fedha Bw Henry Rotich asiipe Serikali pesa za matumizi na hazina ya kustawisha maendeleo katika maeneo bunge (CDF) kabla ya kurekebishwa kwa sheria mpya ya ustawi wa kitaifa-NCDF.

Jaji Joseph Onguto alifahamishwa kwamba agizo la mahakama la kufanyiwa marekebisho kwa sheria ya fedha za kustawisha maeneo ya ubunge (CDF) halijatekelezwa na bunge.

Jaji Onguto alifahamishwa na wakili Suyianka Lempaa kwamba badala ya bunge kurekebisha sheria ya CDF walipitisha sheria ya ustawi wa kitaifa (NGCDF).

Mahakama iliombwa na Taasisi ya Uwajibikaji wa Kijamii (TISA) imwagize Waziri wa Fedha asiachilie pesa zitakazopitishwa na bunge za matumizi katika maeneo ya bunge (CDF) kwa kuwa kuna kizugumkuti katika sheria hizi mbili - CDF na NGCDF.

Rotich na AG kushtakiwa

Jaji Onguto alifahamishwa na wakili Suyianka Lempaa anayemwakilisha Bw Oduor Opuor aliyewashtaki Bw Rotich na Mwanasheria Mkuu, Prof Githu Muigai akishirikiana na Afisa mkuu wa TISA, Bi Wanjiru Gikonyo kwamba hali ya suintofahamu imekumba hazina hizi mbili -CDF na NGCDF- kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Bw Lempaa alimsihi Jaji Onguto apeleke kesi hiyo kwa Jaji Mkuu (CJ) kuteua jopo la majaji watatu au watano kusikiza kesi hiyo iliyoshtakiwa na Bi Gikonyo na Bw Opuot.

Kesi hiyo itaendelea Juni 27.