http://www.swahilihub.com/image/view/-/3262810/medRes/1361464/-/hyim3r/-/kamata.jpg

 

Idadi ya walioshtakiwa wizi wa pesa za NYS yafika watu 30

Patrick Odhiambo Owino

Patrick Odhiambo Owino, mmojawapo wa maafisa wa shirika la huduma ya vijana kwa taifa (NYS) akiwa mahakamani Juni 22, 2016. Picha/RICHARD MUNGUTI 

Na RICHARD MUNGUTI

Imepakiwa - Thursday, June 23  2016 at  00:15

Kwa Muhtasari

Afisa wa shirika la huduma ya vijana kwa taifa (NYS) Jumatano alishtakiwa kwa wizi wa Sh24 milioni.

 

AFISA wa shirika la huduma ya vijana kwa taifa (NYS) Jumatano alishtakiwa kwa wizi wa Sh24 milioni.

Kushtakiwa kwa Patrick Odhiambo Owino kumefikisha idadi ya wafanyakazi na wafanyabiashara waliokabiliwa na mashtaka ya kupora NYS zaidi ya Sh791 milioni kuwa watu 30.

Miongoni mwa wakuu waliofikishwa mahakamani ni pamoja na aliyekuwa katibu wa wizara ya ugatuzi Richard Mangiti na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa NYS Nelson Githinji.

Mfanyabiashara maarufu Ben Gethi aliyeshtakiwa pamoja na Mangiti na Githinji anadhaniwa kuwa mshukiwa mkuu katika kashfa hiyo ya uporaji idara hiyo ya umma.

Dhamana

Bw Owino aliwakilishwa na Bw Samuel Adunda alimuomba hakimu mkazi Bi Joyce Oluoch amwachilie kwa dhamana.

Alikana akishirikiana na wengine walifanya njama za kutenda uhalifu wa kuibia NYS Sh24,145,000 katika taasisi ya Uhandisi kati ya Juni 27 na Agosti 7, 2015.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni pesa taslimu au awasilishe dhamana ya Sh5 milioni.

Kesi itasikizwa Agosti 12, 2016.