'Pocket Rocket' alemewa na mbio za Lisbon Half Marathon

Na  GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, March 20  2017 at  20:48

Kwa Mukhtasari

Wakenya Vivian Cheruiyot na James Wangari Mwangi walizidiwa kasi ya kumaliza mbio na kuridhika katika nafasi za pili za Lisbon Half Marathon nchini Ureno mnamo Machi 19, mtawalia.

 

Bingwa wa Olimpiki mita 5,000 mwaka 2016, Cheruiyot, ambaye anafahamika kwa jina la utani kama Pocket Rocket, alilemewa kwa sekunde moja na bingwa wa marathon duniani Mare Dibaba.

Muethiopia Dibaba alikata utepe kwa saa 1:09:43 naye Cheruiyot alikamilisha umbali huo wa kilomita 21 kwa saa 1:09:44. Mshindi wa Houston Half Marathon mwaka 2016 Mary Wacera kutoka Kenya alishikilia nafasi ya tatu kwa saa 1:09:53.

Mwangi (saa 1:00:11) na Edwin Kibet Koech (1:00:45) walimaliza kitengo cha wanaume katika nafasi za pili na tatu, mtawalia, nyuma ya raia wa New Zealand, Jake Thomas Robertson.      

 

Wanaume

1. Jake Thomas Robertson (New Zealand) saa 1:00:01

2. James Wangari Mwangi (Kenya) 1:00:11

3. Edwin Kibet Koech (Kenya) 1:00:45

4. Tadu Abate Deme (Ethiopia) 1:00:46

5. Nguse Amloson (Eritrea) 1:03:52

6. Samuel Barata (Ureno) 1:03:52

7. Ibrahim Mukunga Wachira (Kenya) 1:04:33

8. Cutbert Nyasango (Zimbabwe) 1:04:36

 

Wanawake

1. Mare Dibaba (Ethiopia) saa 1:09:43

2. Vivian Cheruiyot (Kenya) 1:09:44

3. Mary Wacera (Kenya) 1:09:53

4. Afera Godfay Berha (Ethiopia) 1:09:55

5. Ruti Aga (Ethiopia) 1:10:02

6. Ababel Yeshaneah (Ethiopia) 1:10:13

7. Jessica Augusto (Ureno) 1:10:38

8. Katarzyna Kowalska (Poland) 1:12:01.