http://www.swahilihub.com/image/view/-/2811524/medRes/1074347/-/el4t5m/-/ronaldo.jpg

 

Kumbe Ronaldo alilipa Sh2 bilioni abebewe mimba!

Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo. Picha/MAKTABA 

Na CHRIS ADUNGO

Imepakiwa - Monday, March 20  2017 at  16:23

Kwa Mukhtasari

INGAWA Cristiano Ronaldo yuko katika mahusiano ya kimapenzi na kipusa Georgina Rodriguez, ambaye ni mzawa wa Uhispania, nyota huyo wa Real Madrid anatarajia kuwa baba wa watoto pacha wa kiume watakaozaliwa hivi karibuni na mwanamke mmoja mzawa wa Marekani aliyejitolea kuubeba ujauzito huo.

 

Gazeti la The Sun limesema Ronaldo, 32 aliwahi kutoa mbegu zake za kiume ambazo zilikutanishwa na yai la kichuna mmoja mzawa wa Uhispania aliyelipwa Sh2.8 bilioni kisha mwanamke mmoja mwenye asili ya Amerika akajitolea kuibeba mimba hiyo mwishoni mwa Septemba 2016 kwa kima cha Sh1.5 bilioni.

“Ronaldo ana hamu kubwa ya kuwaona watoto hao ambao watapata hifadhi mpya hivi karibuni katika kasri moja la sogora huyo lenye thamani ya Sh850 milioni jijini Madrid,” ilisema sehemu ya taarifa ya The Sun.

“Dolores ambaye ni mama yake Ronaldo, amejitolea kuwalea wajukuu hao kwa kushirikiana na Georgina ambaye kwa sasa anajivunia uhusiano bora zaidi na Ronaldo Jr ambaye ni mwanambee wa sogora huyo,” ilisema habari kwenye magazeti ya udaku nchini Uhispania huku yakisisitiza kuwa jitihada za kumshawishi Ronaldo kutaja jina la mama wa pacha anaowatarajia zimegonga mwamba.

Mapema mwezi jana, Georgina, 23 alimtaka Ronaldo kufanya hima na kurasimisha uhusiano wao wa kimapenzi ndipo amruhusu kabisa kufurahia joto la mwili wake.

Katika mojawapo ya ziara zao za mara kwa mara za kutalii ufuo wa Ibiza nchini Uhispania, kula ujana na kuponda raha, Georgina alimtajia Ronaldo kuhusu kiu aliyonayo ya kumzalia mtoto atakayedhihirisha ukomavu wa penzi alilonalo kwa sogora huyo mzawa wa Ureno.