http://www.swahilihub.com/image/view/-/4758756/medRes/2109296/-/9x87okz/-/agu.jpg

 

Aguero akamia Ligi Kuu kutwaa kiatu cha dhahabu

Mshambuliaji nyota wa Manchester City, Sergio ‘Kun’ Aguero  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, September 14  2018 at  09:07

Kwa Muhtasari

Amepania kurejesha kiwango cha kufunga mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita

 

London, England. Mshambuliaji nyota wa Manchester City, Sergio ‘Kun’ Aguero amesema yuko fiti kwa mashindano, baada ya kupona jeraha la goti.

Aguero alisema ana amini yuko kwenye kiwango bora na atarudisha makali yake katika Ligi Kuu England.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, alikuwa nje ya uwanja mwezi mmoja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Aguero amefunga mabao matano yakiwemo matatu aliyofunga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Huddersfield.

“Nipo katika hali nzuri sana daktari Ramon Cugat amefanya kazi nzuri katika upasuaji wa goti, kwa sasa najiona nipo kwenye afya njema,”alisema Aguero.

Mchezaji huyo alisema siku chache zilizopita alikuwa kwenye maumivu makali na amepania kurejesha kiwango cha kufunga mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alikuwa tishio kwa mabeki.