Ajowi ataja kikosi kitakachovaana na Ghana

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Thursday, November 2  2017 at  15:12

Kwa Muhtasari

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 ya wanawake, Caroline Ajowi, ametangaza kikosi kitakacholimana na Ghana hapo Novemba 5 mwaka 2017 mjini Cape Coast.

 

Timu hii, ambayo imekuwa ikifanya mazoezi makali uwanjani Kenyatta mjini Machakos, itaelekea nchini Ghana mapema Ijumaa (8.30am) kwa mchuano huu wa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Ufaransa mwezi Agosti mwaka 2018.

Kenya na Ghana zitachuana Novemba 5 (6.30pm) kabla ya kurudiana humu nchini kabla ya Novemba 17.

Warembo wa Ajowi watarejea nchini mapema Novemba 7 (5.30am).

 

Kikosi cha Harambee Starlets

Wachezaji

Corazone Aquino, Judith Osimbo, Wincate Kaari, Brenda Achieng, Diana Wacera, Fiscah Nashivanda, Lilian Awuor, Lucy Akoth, Rachel Muema, Quinter Atieno, Lilian Mmboga, Veronica Awino, Gentrix Shikangwa, Linda Nasimiyu, Leah Cherotich, Martha Amunyolete na Stella Anyango

 

Benchi la kiufundi

Musa Otieno (Mkufunzi), Caroline Ajowi (Kocha Mkuu), Ann Aluoch (Kocha msaidizi), Jackline Akoth (Kocha msaidizi), Hassan Shah (Mkufunzi wa makipa), Mikael Igendia (Kocha wa mazoezi ya viungo vya mwili) na David Ndakalu (Daktari)