Biwot na Barsosio ndio washindi wa mbio za Zagreb Marathon

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, October 9  2017 at  17:47

Kwa Muhtasari

WAKENYA Wycliffe Biwot na Stellah Jepng’etich Barsosio ndio washindi wa mbio za Zagreb Marathon nchini Croatia mwaka 2017.

 

Biwot na Barsosio walihifadhi mataji yao baada ya kukamilisha mbio hizi za kilomita 42 kwa rekodi mpya za Zagreb Marathon za saa 2:09:55 na 2:30:15, mtawalia, Jumapili.

Bingwa wa Budapest Half Marathon nchini Hungary, Biwot, alifuta rekodi ya saa 2:13:10 ambayo Muethiopia Gadisa Birhanu Shumie aliweka mwaka 2015.

Naye Barsosio alivunja rekodi ya saa 2:33:46 ambayo aliweka mwenyewe mwaka 2016.

Wakenya Joel Mwangi na Christine Oigo waliibuka washindi katika kitengo cha mbio za kilomita 21.  

Makala ya mwaka huu, ambayo yalikuwa ya 26, yalivutia maelfu ya washiriki.

 

MATOKEO YA TANO-BORA (Oktoba 8):

Marathon

Wanaume

Wycliffe Biwot (Kenya) saa 2:09:55

Bernard Kitur (Kenya) 2:14:36

Abel Rop (Kenya) 2:15:25

Yavuz Agrali (Uturuki) 2:18:22

Maxim Railenu (Moldova) 2:26:22

 

Wanawake

Stellah Jepng’etich Barsosio (Kenya) saa 2:30:15

Olivera Jevtic (Serbia) 2:35:31

Bojana Bjeljac (Croatia) 2:38:38

Matea Matosevic (Croatia) 2:41:42

Nikolina Sustic (Croatia) 2:46:37

 

Nusu-marathon

Wanaume

Joel Mwangi (Kenya) saa 1:02:09

Hillary Kimaiyo (Kenya) 1:02:19

Nelson Cherutich (Kenya) 1:03:54

Gideon Kosgei (Kenya) 1:04:00

Danijel Fak (Croatia) 1:10:18

 

Wanawake

Christine Oigo (Kenya) dakika 1:11:58

Ruth Matebo (Kenya) 1:13:26

Zita Kacser (Hungary) 1:13:33

Lucija Kimani (Bosnia & Herzegovina) 1:18:37

Tunde Szabo (Hungary) 1:19:39