Black Blad ya K.U yaizima Mombasa

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Sunday, December 3  2017 at  18:39

Kwa Muhtasari

BLAK Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta imevuna ushindi wake wa pili kwenye Ligi Kuu ya Raga ya Kenya kwa kuzaba wenyeji Mombasa kwa alama 22-10 Jumapili.

 

Katika mchuano huu ulioahirishwa kutoka Desemba 2 hadi Desemba 3, Blak Blad ilipata pointi ya bonasi baada ya kufunga miguso minne.

Wafungaji wa miguso ya Blak Blad katika mchuano huu ni Acadius Khwesa, Ian Obukwa, Levy Amunga na Ivan Chebo. Amunga pia alipachika mkwaju mmoja.

Blak Blad imeng’oa Kenya Harlequins kutoka nafasi ya tano baada ya ushindi huu. Imevuna alama tisa nayo Harlequins iko alama mbili nyuma.

Nafasi nne za kwanza zinashikiliwa na Impala Saracens, KCB, Kabras Sugar na Homeboyz, ambazo zimezoa alama 10 kila mmoja.

Mabingwa wa mwaka 2013 na 2014 Nakuru walitupwa chini nafasi tano hadi nambari saba baada ya kuaibishwa 46-19 na Harlequins. Nambari nane Mwamba imezoa alama moja nazo Nondies, Mombasa, Kisii na Strathmore Leos hazina alama.

 

Matokeo:

Desemba 2

Mwamba 12-30 Impala Saracens

Kenya Harlequins 46-19 Nakuru

Kabras Sugar 44-13 Strathmore Leos

Homeboyz 29-21 Nondies

Kisii 6-33 KCB

 

Novemba 28

Homeboyz 41-39 Kenya Harlequins

 

Novemba 25

Nakuru 45-15 Kisii

Impala Saracens 48-0 Mombasa

Strathmore Leos 0-27 KCB

Kabras Sugar 29-22 Mwamba

Blak Blad 8-0 Nondies