Cheptegei alemewa kuvunja rekodi ya Mkenya mwenzake

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, November 20  2017 at  17:19

Kwa Muhtasari

MGANDA Joshua Cheptegei alifeli katika lengo lake la kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 15 ya dakika 41:13 inayoshikiliwa na Mkenya Leonard Komon mjini Nijmegen nchini Uholanzi hapo Novemba 19, 2017.

 

Cheptegei alikamilisha shindano la Zevenheuvelenloop wa kwanza kwa dakika 41:17, sekunde nne nje ya rekodi iliyowekwa na Komon katika shindano hili mwaka 2010.

Kabla ya kushiriki shindano hili, Cheptegei aliapa kufuta rekodi ya Komon. Baada ya mbio alisema, “Nasikitika sikuvunja rekodi ya Zevenheuvelenloop ambayo ilikuwa lengo langu kubwa. Hata hivyo, nafurahia kuibuka mshindi na ninatumai kurejea hapa miaka ijayo kujaribu tena kuvizia rekodi hiyo.”

Cheptegei alifuatwa kwa karibu na Muethiopia Amdework Welelegn (dakika 42:40) naye Mkenya Noah Kipkemboi akafunga mduara wa tatu-bora (42:43).

 

Matokeo (Novemba 19, 2017):

Wanaume

Joshua Cheptegei (Uganda) dakika 41:17

Amdework Welelegn (Ethiopia) 42:40

Noah Kipkemboi (Kenya) 42:43

Yenew Alamirew (Ethiopia) 43:33

Mekonnen Gebremedhin (Ethiopia) 43:35

Joseph Katib (Uganda) 43:36

Biya Simbassa (Marekani) 43:37

Victor Chumo (Kenya) 43:43

Phielemon Kacheran (Kenya) 44:27

Callum Hawkins (Marekani) 44:45