Ethiopia yaibandua Kenya New York City Marathon

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, March 20  2017 at  20:42

Kwa Mukhtasari

Utawala wa miaka mitano wa Kenya katika mbio za kilomita 21 za wanaume za New York City Marathon ulifikia ukingoni nchini Marekani mnamo Jumapili.

 

Kenya ilikuwa imeshinda kitengo hiki kupitia Peter Kirui (2012), Wilson Kipsang’ (2013), Geoffrey Mutai (2014), Leonard Korir (2015) na Stephen Sambu (2016) kabla ya Muethiopia Feyisa Lilesa kunyakua taji la mwaka 2017.

Sambu, ambaye alikuwa akitetea taji alikuwa Mkenya wa pekee ndani ya wakimbiaji 19-bora. Alimaliza katika nafasi ya nne kwa saa 1:00:55.  

Muamerika Molly Huddle alishinda taji la wanawake kwa mwaka wa tatu mfululizo. Wakenya wawili walimaliza ndani ya 10-bora.

Bingwa wa marathon duniani mwaka 2011 na 2013 Edna Kiplagat alikamilisha mbio hizi katika nafasi ya nne naye bingwa wa New York City Half Marathon mwaka 2011 na 2013 Caroline Rotich akaambulia nafasi ya tisa.


Matokeo (Machi 19):

Wanawake: 1.Molly Huddle (Marekani) saa 1:08:19, 2.Emily Sisson (Marekani) 1:08:21, 3.Diane Nukuri (Burundi) 1:09:13, 4.Edna Kiplagat (Kenya) 1:09:37, 10.Caroline Rotich (Kenya) 1:12:09

 

Wanaume: 1.Feyisa Lilesa (Ethiopia) saa 1:00:04, 2.Callum Hawkins (Uingereza) 1:00:08, 3.Teshome Mekonen (Ethiopia) 1:00:28, 4.Stephen Sambu (Kenya) 1:00:55.