http://www.swahilihub.com/image/view/-/4927044/medRes/2187067/-/nsf8f/-/sir+alex.jpg

 

Ferguson awapasha mastaa Man United

Sir Alex Ferguson 

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Wednesday, January 9  2019 at  08:44

Kwa Muhtasari

Kundi hili lina uwezo wa kufanya mabadiliko na kuiletea sifa United

 

 

London, England. Sir Alex Ferguson amewaeleza wachezaji wa Manchester United watarudisha hadhi ya klabu hiyo kama ilivyokuwa enzi zake.

Pia Ferguson amesema atampa kila aina ya ushirikiano kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer, katika kampeni yake ya kuisuka upya Man United.

Kauli ya kocha huyo wa zamani wa timu hiyo mwenye historia ya pekee, imekuja muda mfupi baada ya Solskjaer kushinda mechi tano mfululizo dhidi ya Cardiff City, Huddersfield, Bournemouth, Newcastle United na Reading.

Nguli huyo alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa timu hiyo ana nafasi ya kurudisha hadhi ya Man United katika ramani ya soka kwa kuwa ana wachezaji bora.

Ferguson amewataka wachezaji kuipigania Man United katika mechi zote za mashindano kwa kuwa wana uwezo na viwango bora vya kucheza soka.

Kocha huyo alitoa kauli hiyo alipoalikwa na Solskjaer kwenda uwanjani kuzungumza na wachezaji ikiwemo kuwajengea uwezo wa kujiamini katika mechi za mashindano.

“Kundi hili lina uwezo wa kufanya mabadiliko na kuiletea sifa United, naamini wakipambana uwanjani mambo yatakuwa mazuri,” alisema Ferguson. Ferguson mwenye miaka 77, alisema yuko tayari kuzungumza na wachezaji masuala ya kiufundi kila watakapokuwa wakimuhitaji. Nguli huyo alianza kuinoa Man United mwaka 1986 hadi 2013.