Harlequins washinda Driftwood Sevens Raga za Kitaifa

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Sunday, August 21  2016 at  19:32

Kwa Muhtasari

Kenya Harlequins wametawazwa mabingwa wa duru ya tatu ya Raga za Kitaifa za wachezaji saba kila upande ya Driftwood Sevens iliyokamilika mjini Mombasa, Jumapili.

 

KENYA Harlequins wametawazwa mabingwa wa duru ya tatu ya Raga za Kitaifa za wachezaji saba kila upande ya Driftwood Sevens iliyokamilika mjini Mombasa, Jumapili.

Quins walitoka nyuma 0-7 na tena 7-14 kabla ya kupiga mabingwa wa duru ya Prinsloo Sevens Homeboyz 19-14 katika fainali kali na ya kusisimua.

Strathmore Leos walikamata nafasi ya tatu baada ya kulima Kabras Sugar 12-7. Mabingwa watetezi wa Raga za Kitaifa zinazojumuisha duru sita mwaka 2016, KCB wamelemea mabingwa wa Kabeberi Sevens Impala Saracens 17-5 katika fainali ya Sahani.

Nakuru ndiyo mabingwa wa Bakuli. Wamelaza Menengai Oilers 14-0 nao Daystar wameridhika na taji la Ngao baada ya kushinda Kisii 26-5.

 

MATOKEO (Agosti 21)

Robo-fainali ya Bakuli

Nakuru 29-0 Daystar

Mean Machine 29-5 Mombasa

Makueni 7-5 Kisumu

Kisii 0-5 Menengai Oilers

 

Robo-fainali Kuu

Blak Blad 5-19 Quins

Strathmore Leos 19-12 KCB

Kabras Sugar 8-5 Impala Saracens

Homeboyz 20-5 Mwamba

 

Nusu-fainali ya Ngao

Daystar 7-5 Mombasa

Kisumu 27-0 Kisii

 

Nusu-fainali ya Bakuli

Nakuru 12-0 Mean Machine

Makueni 0-17 Menengai Oilers

 

Nusu-fainali ya Sahani

Blak Blad 0-17 KCB

Impala 5-0 Mwamba

 

Nusu-fainali Kuu

Quins 14-0 Strathmore Leos

Kabras Sugar 12-19 Homeboyz

 

Fainali ya Ngao

Daystar 26-5 Kisii,

 

Fainali ya Bakuli

Nakuru 14-0 M.Oilers

 

Fainali ya Sahani

KCB 17-5 Impala

 

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu

Strathmore Leos 12-7 Kabras

 

Fainali Kuu

Quins 19-14 Homeboyz