http://www.swahilihub.com/image/view/-/4610480/medRes/2007583/-/ap4xoo/-/rapa.png

 

Hilter alaani habari za kuzushiwa kifo

Rapa wa Bendi ya FM Academia, Hitler Norma Benga aliyezushiwa kifo  

Na Rhobi Chacha

Imepakiwa - Wednesday, June 13  2018 at  15:48

Kwa Muhtasari

Hitler ameweka wazi kwamba yupo hai na ameshangaa kuzushiwa habari za kifo

 

Rapa anayeitumikia Bendi ya FM Academia anayejulikana Hitler Norma Benga ‘Hitler’ amezushiwa kifo, hata hivyo kiongozi msaidizi wa bendi hyo amethibitisha msanii huyo yupo hai.

Leo asubuhi taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, radio na televisheshi zikidai kuwa  Hilter amefariki kwa ajali ya pikipiki Kibaha mkoani Pwani.

Hitler ameweka wazi kwamba yupo hai na ameshangaa kuzushiwa habari za kifo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema alishangazwa kusikia watu wakizungumzia taarifa za kifo chake baada ya marafiki zake kukusanyika nyumbani kwake Mwananyamala Kwa Kopa jijini Dar es Salaam.

Pia kiongozi Msaidizi wa Bendi ya FM Academia, Christian Mene, amezingumza na Mwanaspoti na kusema kuwa Hilter ni mzima wala hahusiki na ajali hiyo.

“Kwanza tunawapa pole ndugu zetu wote waliopata usumbufu wa taarifa hizi za Hitler kuwa amefariki. Ukweli ni kwamba hajafariki.”