Jane Wacu aeleza sababu ya kuichezea klabu ya Ushelisheli

 Jane Wacu

Jane Wacu. Picha/MAKTABA 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Friday, August 11  2017 at  08:56

Kwa Mukhtasari

Nyota wa voliboli nchini Jane Wacu kasema alikuwa na sababu sahihi kuitosa dili ya kujiunga na Kenya Pipeline na kukimbilia zake ughaibuni.

 

NYOTA wa voliboli nchini Jane Wacu kasema alikuwa na sababu sahihi kuitosa dili ya kujiunga na Kenya Pipeline na kukimbilia zake ughaibuni.

Kichuna huyo kaangukia bonge la dili kuichezea klabu moja ya Ushelisheli (Seychelles).

Wacu zamani akiichezea Kenya Prisons alikuwa kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Kenya Pipeline ilipotokea dili hiyo ya kucheza nje ya nchi.

Ofa aliyokuwa akipewa ya Sh3.5 milioni kwa mwaka ikambadili mawazo Wacu mwenye miaka 32, na kuamua kuwatosa Kenya Pipeline na mara moja kupanda ndege na kuelekea zake huko Ushelisheli kukamlisha dili hiyo.

“Kabla sijaikubali ofa hiyo niliketi chini nikawaza sana na mwisho wa siku nilifanya uamuzi ninaohisi utanifaa. Wajua sitakuwa mchezaji daima hivyo ni lazima niyaangalie maisha yangu ya usoni na kwa dili kama ile kwa misingi hiyo ingekuwa vigumu mimi kuikataa,” aliiambia safu hii.