Jeruto amaliza nafasi ya 5 mashindano ya Miss World

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Sunday, November 19  2017 at  19:18

Kwa Muhtasari

MKENYA Magline Jeruto amemaliza mashindano ya urembo ya dunia (Miss World) katika nafasi ya tano kutoka orodha ya wanamitindo 118 walioshiriki mwaka 2017.

 

Mshindi huyu wa tuzo ya Miss World Kenya alimaliza katika nafasi ya kwanza barani Afrika.

Raia wa India, Manushi Chhillar alitawazwa malkia wa dunia mwaka 2017 katika hafla iliyoandaliwa mjini Sanya nchini Uchina hapo Novemba 18, 2017.

Nambari mbili na tatu ziliwaendea Andrea Meza wa Mexico na Muingereza Stephanie Hill, huku Jeruto akimaliza nyuma ya Mfaransa Aurore Kichenin.

Ni mara ya pili mfululizo Mkenya amemaliza mashindano haya ya kila mwaka ndani ya mduara wa tano bora baada ya Evelyn Njambi kushikilia nafasi ya nne mwaka 2016.