Johanna azidi kutamba nchini Uswidi

Na CHRIS ADUNGO

Imepakiwa - Tuesday, October 24  2017 at  13:06

Kwa Muhtasari

NYOTA wa zamani wa Mathare United, Eric Johanna 'Maapake’ Omondi ni miongoni mwa Wakenya wanaozidi kung’arisha nyota zao katika soka ya ughaibuni baada ya kupachika wavuni mabao matatu yaliyowachochea waajiri wake Vasalund kuwabamiza IFK Lulea 4-0 katika Ligi ya Daraja la Pili nchini Uswidi.

 

Maapake alifunga mabao mawili ya haraka katika kipindi cha pili baada ya Linus Malmborg kuwafungulia Vasalund ukurasa wa mabao kunako dakika ya 17 katika mchuano huo uliotandazwa mnamo Oktoba 22, 2017.

Nicolas Payvey alikizamisha kabisa chombo cha wapinzani wao kwa kufunga bao la nne dakika saba kabla ya kipenga cha mwisho wa kipindi cha pili kupulizwa.

Licha ya mafanikio hayo, ushindi wa Vasalund haukotosha kuwaondoa katika mduara wa hatari jedwalini hasa ikizingatiwa kwamba wanashikilia nafasi ya 18 kwenye orodha ya vikosi 20 vinavyonogesha kampeni za Ligi ya Daraja la Pili nchini Uswidi.

Ushindi wa waajiri hao wa Maapake ulikuwa wa kwanza kwa wao kusajili baada ya kuzidiwa maarifa na wapinzani kutokana na michuano mitano iliyopita mfululizo.