http://www.swahilihub.com/image/view/-/4802360/medRes/2138178/-/12jhy4iz/-/ram.jpg

 

Juventus yampandia dau Ramsey

Kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, October 12  2018 at  08:57

Kwa Muhtasari

Inataka kutengeneza mazingira ya kumnasa kwa kumpa mkataba

 

London, England. Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin imeongeza kasi ya kuwania saini ya kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwakani.

Juventus ina matumaini ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales akiwa huru, baada ya mkataba wake kumalizika.

Ramsey aliyegeuka gumzo siku za karibuni kwa kufunga bao la kisigino dhidi ya Fulham, pia anawindwa na Liverpool ya England.

Juventus ina matumaini ya kupata saini ya mchezaji huyo kwa kuwa atakuwa huru mwishoni mwa msimu huu, lakini inataka kutengeneza mazingira ya kumnasa Januari kwa kumpa mkataba wa awali.

Ramsey anapewa nafasi ya kumwaga wino Juventus kwa kutia saini mkataba wa awali baada ya Arsenal kushindwa kumpa dau analotaka katika maboresho ya mkataba mpya.

Ramsey anataka mshahara wa Pauni250 kwa wiki jambo ambalo limemuweka njia panda kocha Unai Emery.

Juventus, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Italia, wako mbele pointi sita dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili na inanolewa na kocha nguli Massimiliano Allegri .

Liverpool na Chelsea zinafuatilia kwa karibu mkataba wa Ramsey aliyeonyesha nia ya kucheza pembeni mwa nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo.