Kocha Aussems atanguliza jeshi Dar

Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems 

Imepakiwa - Wednesday, January 9  2019 at  12:35

Kwa Muhtasari

Atanguliza kikosi cha wachezaji 17

 

 

Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems ametanguliza jeshi lake jijini Dar es Salaam ambapo yeye ataondoka mchana wa leo Jumatano pamoja na familia yake.

Aussems alitanguliza kikosi cha wachezaji 17 huku yeye, mke na watoto wake wawili wakifuata na boti ya mchana.

Msafara wa kwanza uliongozwa na daktari wa timu,  Yassin Gembe, kocha wa makipa Mohamed Muharami, kocha wa viungo Zrene Adel na mtunza vifaa Hamis Mtambo.

Wachezaji walioondoka ni John Bocco, Aishi Manula, Shiza Kichuya, Meddie Kagere, Nicolas Gyan, Pascal Wawa, Clatous chama na Emmanuel Okwi ambaye aliondoka wa kwanza ambapo alitumia usafiri wa Ndege.

Wengine ni Haruna Niyonzima, James Kote, Deigratius Munishi, Hassan Dilunga, Juuko Murshid, Rashid juma, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin na Said