http://www.swahilihub.com/image/view/-/4612012/medRes/2008647/-/i8eim5/-/lena.jpg

 

Kombe la Dunia kupambwa na warembo

Lena Gercke, mke  wa Sami Khedira wa Ujerumani  

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Thursday, June 14  2018 at  13:03

 

SUBIRI wewe. Utamu wa fainali za Kombe la Dunia huko Russia si kwenda kumwona tu Lionel Messi na mwenzake Cristiano Ronaldo wakifanya yao, lakini ni kushuhudia pia warembo matata kabisa watakaokuwa jukwaani kuwashangilia wanasoka hao.

Unaambiwa hivi, kazi na dawa. We unadhani Neymar atakipiga kwa nguvu kiasi gani ndani ya uwanja atakapogundua yule mrembo wake anayemkubali kupita wote yupo jukwaani anamtazama na kumshangilia?

Fainali hizo za Russia zitahusisha wanasoka 736 na hakuna ubishi, wengi wao wataandamana na wachumba na wake zao kwenye kunogesha zaidi michuano hiyo.

Lakini, unaambiwa hivi, panga pangua kuna wachumba wa wanasoka hao, hawawezi kukosa kwenye fainali hizo za Russia kutokana na ukweli kwamba wamekuwa na kawaida ya kuwasapoti wanaume zao wanapokuwa na mechi ngumu na muhimu kama hizo za kusaka ubingwa wa dunia.

Usishangae kuona kunakuwapo kwa usaliti pia kwa wanawake hao kisa wanaume zaidi kama itakavyotokea kwa mwimbaji mrembo kabisa, Shakira, ambaye taifa lake la Colombia litakuwapo kwenye fainali hizo, lakini sasa anatazamiwa kuwa bega kwa bega na mpenzi wake, Gerard Pique, ambaye ni beki wa kati wa Hispania.

Mabinti wengine matata ambao huwezi kuwakosa kwenye fainali hizo za Russia, wakienda kuwasapoti waume zao ni pamoja na Georgina Rodriguez, atakayekuwa jukwaani kumshangilia Ronaldo na Ureno yake, huku mrembo matata kabisa Ruby Mae, akitarajia kutokosa mechi hata moja za England ili kwenda kumshangilia kipenzi chake Dele Alli, kama itakavyokuwa kwa mrembo Sara Salamo, ambaye hatahitaji kusimuliwa kuhusu mechi za Hispania ili amwone tu mtu wake, Isco.

Mrembo Lena Gercke hatazamiwi kukosa pia kutokana na mke huyo wa Sami Khedira wa Ujerumani kuwa na kawaida ya kwenda kumshangilia mume wake anapokuwa kazini, huku Yuri Zhirkov, atakuwa na hamasa kubwa kutoka kwa mrembo Inna Zhirkova, wakati supastaa wa Ufaransa, Antoine Griezmann akitatarajia kuwa kwenye mapenzi motomoto ya kushangiliwa na mrembo wake, Erika Choperena.

Mrembo Bruna Marquezine wa Neymar hawezi kukosa, sawa na Antonella Roccuzzo wa Messi, Andrea Duro wa Chicharito, Edurne wa David De Gea, Anastasia Kostenko wa staa wa Russia, Dmitri Tarasov, Helga Lovekaty mchumba wa James Rodriguez wa Colombia, ambaye atakuwa tofauti na Shakira, atakayekuwa sapoti kubwa kwa Pique wa kikosi cha La Roja.