http://www.swahilihub.com/image/view/-/4924092/medRes/2217113/-/y25ugq/-/saleh.jpg

 

Kwa hii Yanga! Simba inasubiri

Mratibu wa Yanga, Saleh Hafidh 

Na Mwanahiba Richard

Imepakiwa - Monday, January 7  2019 at  08:54

Kwa Muhtasari

Msimu wote huu tumetumia jezi mpya maana tulikuwa nazo nyingi sana

 

NI kweli Yanga imekuwa ikitegemea bakuli la mashabiki wake kuendesha baadhi ya mambo, huku Kocha wake, Mwinyi Zahera kuna wakati akijipapasa mfukoni ili kuokoa jahazi, lakini asikuambie mtu, jamaa wamefunika mbaya.

Ndio, katika Ligi Kuu, licha ya kuongoza kileleni, lakini Yanga pia inaongoza kwa kuwa na jezi nyingi ilifanya kufuru kwa kubadilisha uzi karibu kila mechi na hasa michuano tofauti.

Hata huku Unguja, wababe hao wakishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi bado imetisha kwa kutinga ikiwa na seti nne za jezi na tayari mbili imeshatumia katika mechi zao dhidi la KVZ na Azam.

Huenda leo watakapovaana na Malindi watashuka Uwanja wa Amaan na uzi mwingine kwani, mechi yao ya KVZ walitumia jezi zenye rangi ya kijani na njano zinafanana kidogo na uzi wa timu ya Taifa ya Nigeria kasoro rangi tu.

Juzi Jumamosi walipoivaa Azam na kulala mabao 3-0 walitinga uzi wa kijana wenye ufito wa njano kifuani.

Mratibu wa Yanga, Saleh Hafidh aliliambia Mwanaspoti wana jezi nyingi ambazo ni zaidi ya tano mpya na hadi sasa ni mbili tu zimebaki.

“Msimu wote huu tumetumia jezi mpya maana tulikuwa nazo nyingi sana, tuna nyeusi, njano na kijani kasoro namna zilivyotengenezwa ni aina tofauti tofauti.

“Ukiachana na jezi pia tuna ‘track suit’ za aina mbalimbali ambazo pia ni mpya, na zote ni orijino hakuna feki, jezi zetu zinatengenezwa na kampuni ya Nike, alisema Hafidh.

Wakati Hafidh akielezea hilo kuhusu utajiri wa jezi, meneja Nadir Haroub ‘Canavaro’ naye alitamba kwamba “Simba wametuzidi pesa tu lakini kwa jezi hawatufikii, tuna jezi nyingi mpya na orijino hatutaki vitu feki, tunaongoza ligi na jezi pia.