Malkia Strikers watua Yaounde tayari kupigania tiketi

Na  GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Thursday, October 5  2017 at  19:07

Kwa Muhtasari

TIMU ya taifa ya voliboli ya wanawake ya Kenya imetua salama salmini jijini Yaounde, Cameroon, Alhamisi jioni.

 

Malkia Strikers inavyofahamika kwa jina la utani, iliondoka jijini Nairobi mapema Alhamisi ikitumia ndege ya Ethiopian Airlines.

Kutoka Nairobi, Malkia Strikers, ambayo inanolewa na makocha Japheth Munala na David Lung’aho, ilielekea jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kabla ya kufunga safari ya Cameroon.

Timu hiyo itakuwa nchini Cameroon kwa juma moja ikipigania tiketi ya kuwakilisha Bara Afrika katika mashindano ya dunia nchini Japan mnamo Septemba 29 hadi Oktoba 20 mwaka 2018.

Mataifa yatakayowania ubingwa wa Afrika na tiketi hiyo moja ya kushiriki mashindano ya dunia ni Kenya, Misri, Algeria, Tunisia, Botswana, Cameroon, Cape Verde, Ghana, Madagascar, Nigeria, Senegal na Ushelisheli.