http://www.swahilihub.com/image/view/-/2829022/medRes/1087937/-/7ey3fnz/-/malkia.jpg

 

Kocha wa Malkia Strikers atahadharisha wapinzani

Malkia Strikers

Timu ya taifa ya voliboli kwa kina dada Malkia Strikers ilipowasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) Julai 14, 2015 kutoka Australia. Picha/MARTIN MUKANGU 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Wednesday, August 12  2015 at  08:38

Kwa Muhtasari

Kocha wa timu ya taifa ya voliboli kwa wanawake, Malkia Strikers, David Lung’aho ametangazia wapinzani hali ya hatari, kikosi chake kinapozidi kujianda kuondoka nchini, kuelekea Japan ambapo kitashiriki dimba la dunia la mchezo huo FIVB 2015.

 

KOCHA wa timu ya taifa ya voliboli kwa wanawake, Malkia Strikers, David Lung’aho ametangazia wapinzani hali ya hatari, kikosi chake kinapozidi kujianda kuondoka nchini Jumatano, kuelekea Japan ambapo kitashiriki dimba la dunia la mchezo huo FIVB 2015.

Shindano hilo litang’oa nanga rasmi Agosti 22 hadi Septemba 6 lakini kikosi hicho kimeamua kusafiri mapema ambapo kitakuwa Japan wiki moja kabla ya kuanza kwa mashindano.

Hivyo timu hiyo itakuwa na muda mzuri wa kukoleza mazoezi yao kando na kujifahamisha na mdhadhari ya taifa hilo ikiwemo pia hali ya anga, jambo ambalo kwa asilimia kubwa huchangia matokeo.

Kenya haijakuwa ikifanya vyema kwenye mashindano ya dunia lakini safari hii kocha Lung’aho ameshikilia kuwa mambo yatakuwa tofauti sana kwa kuwa amekipevusha na kukiboresha kikosi chake kuliko kilivyokuwa hapo zamani.

“Katika miaka ya nyuma, tumekuwa tukishiriki makala ya voliboli ya duniani FIVB kama tu washirika. Yaani tunakuwa tu pale kukamilisha idadi ya timu zinazohitajika kuwa kwenye shindano. Ila safari huii natahadharisha kwamba hatwendi kule kushiriki tu, mbali kutoa ushindani wa uhakika ili tuwashangaze wengi am,bao wamekuwa wakituchukulia maboya” Lung’aho akakata kauli.

Kenya haijakuwa ikifanya vyema kwenye makala ya awali katika ngaziu hiyo ya duniani licha ya kufanya vizuri barani Afrika wakiwa ndio mabingwa mara tisa wa Afrika. Hata hivyo mwaka huu kwa maneno yake mweyewe kocha, kikosi kinaonekana kuwa kimekaa vizuri hasa baada yacho kushinda fainali ya kwenye kundi la tatu la FIVB Grand Prix kule Australia mwezi uliopita.

Kocha Lung’aho amefanya mabadiliko mawili katika kikosi chake hicho kwa kuwajumulisha wanadhoruba wa klabu ya KCB, Farida Efumbi na Bilha Jepchirchir.

Mara ya kwanza 2004

Idadi kubwa ya wachezaji wa Malkia Stars wakiongozwa na nahodha mzoefu, Praxcides Agala pamoja na msaidizi wake, waliitwa kikosini kwa mara ya kwanza 2004.

Malkia Stars watakuwa wakishiriki dimba hili la dunia kwa mara ya tano watakakokuwa wakisaka ushindi wao wa kwanza. Kwenye makala ya kwanza 1991 yaliyoandaliwa kuko huko Japan, Kenya ilimaliza katiuka nafasi ya 12. Miaka minne baadaye ikapanda hasdi nafasi ya 11 kabla ya kuteremka hadi nambari 12 kwenye makala yaliyofuatia ya 2007 na 2011.

Kenya itafunguia dimba dhidi ya taifa la Cuba kwenye siku ya kwanza ya kuanza kwa shindano, kisha siku ya pili itachuana na Dominican Repbulic huku mchuano wa tatu ukiwakutanisha na Urusi. Mechi ya nne watapambana na wenyeji Japan.

KIKOSI: Praxcides Agala, Ruth Jepng’etich, Monica Biama, Noel Murambi, Mercy Moim, Jane Wacu, Everlyn Makuto, Janet Wanja, Farida Efumbi, Bilha Jepchirchir, Elizabeth Wanyama, Lydia Maiyo, Easther Wangeci, Triza Atuk