http://www.swahilihub.com/image/view/-/4915686/medRes/2211554/-/aqn5vm/-/ole.jpg

 

Martial, De Gea wamchokonoa Solskjaer

Ole Gunnar Solskjaer   

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Monday, December 31  2018 at  09:57

Kwa Muhtasari

Wachezaji wanatakiwa kuwa wapole

 

Manchester, England. Inaonekana hawa jamaa watu wa mizengwe sana. Amini usiamini siku chache baada ya Ole Gunnar Solskjaer kupewa timu kuisimamia kwa muda, kipa wa timu hiyo, David de Gea na Anthony Martial wamelianzisha na tayari wameonywa.

Ole Gunnar Solskjaer aliwaonya wachezaji hao waliokuwa wakizungumza chinichini masuala yao ya kutimka klabuni.

De Gea mkataba wake unamalizika 2020 na anataka kujadiliwa na anataka pia malipo zaidi Manchester United kabla ya kusaini mkataba mpya.

Martial, naye yuko kwenye mpango wa kusepa United lakini alikuwa akipozwa na Jose Mourinho na sasa anataka kusaini mkataba mpya. Solskjaer anaamini kuwa wachezaji hao watabakia tu Old Trafford.

‘Ninafahamu kuwa klabu inawataka kusaini, of course, ni wachezaji wazuri,’ Solskjaer alisema kabla ya mechi yao ya jana dhidi ya Bournemouth, pale Old Trafford. ‘Wachezaji wanatakiwa kuwa wapole, hii ya kuwapo Man United tu, tayari mambo yako ni safi, sasa hayo mengine yatarekebishwa.

“Uko pazuri. Uko klabu kubwa duniani. ‘Nitalisimamia suala lao kuona wanabakia muda mrefu klabuni. ‘Kama unapangwa mara kwa mara Manchester United, unatakiwa kusimamia nafasi yako kuona unapata heshima ya kupangwa.

‘Mimi mwenyewe nina ofa nyingi na watu wengi wa kusajili lakini [Sir Alex Ferguson] ameniambia nitakuwa mtu muhimu hapa kwenye timu, na tutacheza mechi nyingi tu nivute subira.”