Mashabiki wanaofanya vitendo vya kihuni waonywa

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May  

Imepakiwa - Tuesday, July 10  2018 at  16:30

Kwa Muhtasari

Mashabiki wengi hunywa pombe kupita kiasi

 

London, England. Ofisa anayehusika na Usalama ndani ya Chama cha soka England, amerejea wito wa Polisi wa Uingereza, kuwaonya mashabiki wa nchi hiyo kutojihusisha na uhuni wowote wawapo nchini Russia.

Alisema FA haitawafumbia macho katika hilo, watahakikisha wanawachunguza na kuwakamata mashabiki wote watakaofanya vitendo vya kihuni katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia itakayopigwa leo ikizikutanisha England na Croatia nchini Russia.

Ofisa huyo,

hilo limetolewa baada ya mashabiki hao walioonyesha vitendo vya kihuni na kuhatarisha usalama wao wakati na baada ya mechi ya robo fainali dhidi ya Sweden.

Alisema serikali ya Uingereza chini ya waziri Mkuu, Theresa May, imeonya mara kadhaa kuhusu uhuni wa mashabiki unavyoweza kuleta maafa kwenye taifa hilo, lakini inaonekana onyo hilo limekua likipuuzwa, kutokana na mashabiki wengi kunywa pombe kupita kiasi kabla ya kwenda uwanjani.

“Hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayejihusisha kwa namna yoyote ile na ghasia nchini Russia iwe ni kabla ya mechi, wakati wa mechi au baada ya mechi, kwa hakika katika hili tutatumia kila aina ya utafiti kuwanasa wote watakaojihusisha na vurugu,” alisisitiza.

 

&&&&

Neymar awakasirikia mashabiki

Rio de Janeiro, Brazil. Nahodha wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar, ameonyesha hasira zake kwa mashabiki baada ya kuwakimbia kwenye uwanja wa ndege mjini Rio de Janeiro.

Maelfu ya mashabiki walijitokea kuilaki timu yao iliyorejea nyumbani baada ya kuondolewa na Ubelgiji katika robo fainali ya Kombe la Dunia linaloendelea nchini Russia.

Msafara wa Brazil, ulirejea mjini Rio de Janeiro, Jumapili huku matarajio ya mashabiki wengi kutaka kumuona nahodha wao Neymar anayekipiga Paris Saint Germany (PSG) ya Ufaransa, yakiyeyuka.

Ulinzi uliimarishwa uwanjani hapo, baada ya kadhia waliyoipata mjini Madrid Hispania walikopopolewa kwa mayai visa, Hata hivyo mashabiki hao walipigwa na butwaa baada ya kutomuona Neymar.

Msafara wa wachezaji na viongozi ulipotoka na mashabiki na wanahabari wengi kiu yao ili kumuona na kumsikia Neymar lakini walijikuta wakibaki njia panda baada ya Neymar kutoonekana.

Baadaye wafanyakazi wa uwanja wa ndege walivujisha kuwa Neymar alikua wa kwanza kushuka na alitokea kusikojulikana akipitia mlango maalum, wakitaka kumhoji lakini e kutoka nje ya uwanja na kuanza kuingia kwenye gari tayari kuondoka uwanjani hapo.

Mashabiki hao waliishia kuwaona wachezaji wengine na kuwaomba wasaini kwenye jezi na vijitabu vyao, wakiwemo Casemiro, Douglas Costa, Gabriel Jesus, Geromer, Philippe Coutinho,  Taison na wengine laki hawakumuona Neymar.

Hata hivyo ilifahamika baadaye kuwa Neymar alitokea mlango wa uwani na kutokomea zake akiwaacha mashabiki na wanahabari kwenye mataa.

Mshambuliji mahiri wa zamani wa Brazil, Ronaldo de Lima, alisema hamlaumu Neymar, kwa alichokifanya kwani alikua ameumizwa kwa kutolewa na namna mashabiki walivyoishia kuwalaumu badala ya kuwapongeza.

Ronaldo alisema kufika robo fainali ni hatua nzuri inayostahili pongezi licha ya kwamba matarajio yalikua kutwaan ubingwa.

&&&

Uruguay bado hawaamini

Montevideo, Uruguay. Nahodha wa Uruguay, Diego Godin, amewashukuru mashabiki wa nchi hiyo kwa kuwaunga mkono wakati wote wa ushiriki wao kwenye fainali za 21 za Kombe la Dunia.

Godin alisisitiza kuwa timu yao ndiyo ilikua bora zaidi katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia, licha ya kutolewa kabla ya kutimiza kiu cha muda mrefu cha kutwaa ubingwa.

Alisema hadi sasa wachezaji bado hawaelewi ilikuwaje wakafungwa mabao 2-0 na Ufaransa katika mechi ya robo fainali na kutupwa nje ya fainali hizo za Kombe la Dunia 2018 zinazoendelea nchini Russia.

Mabao ya Raphael Varane dakika ya 40 na Antoine Griezmann dakika ya 61, kwenye uwanja wa Nizhny Novgorod ndiyo yaliyomaliza safari ya Uruguay kusaka taji hilo walilolikosa tangu mwaka 1950.

Mabingwa hao wa kwanza wa Kombe la Dunia walilolitwaa mwaka 1930 wakiwa wenyeji, walikua miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kulitwaa taji ka mwaka huu lakini haikua hivyo.

“Kwa kweli Uruguay ilikua timu bora kabisa katika fainali za mwaka huu Kombe Dunia, hata hivyo tunasema ni bahati mbaya sana tumetolewa kwenye robo fainali,” alisema.

Mlinzi huyo wa Atletico Madrid ya Hispania, alisema kuwa pamoja na kuugulia maumivu ya kutolewa ambayo bado hawaamini mpaka sasa lakini wanawashukuru mashabiki kwa namna walivyowaunga mkono na wanawaomba waendelee kufanya hivyo.

Alisema kwa sasa wachezaji wote wana machungu na watarekebisha makosa yao na watawapooza machungu mashabiki wao kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Amerika Kusini na michuano mingine watakayoshiriki.

Alisema wanaamini wametolewa kwa kukosa bahati lakini sio kucheza chini kiwango hivyo wanaomba radhi, hata wao wameumia sana kwa kutolewa huko, ila wanaahidi kupambana zaidi katika michuano iliyo mbele yao.