Mchezaji Bora Afrika: Olunga atemwa

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, November 13  2017 at  15:18

Kwa Muhtasari

MKENYA Michael Olunga ameondolewa katika mbio za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa soka wa Afrika mwaka 2017.

 

Kutoka orodha ya kwanza ya wapigaji soka 30, Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limepunguza majina hadi watano, huku Olunga akiwa mmoja wao waliotupiliwa mbali.

Wachezaji waliosalia mbioni ni Mohamed Salah (Misri na Liverpool), Naby Keita (Guinea & RB Leipzig), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Victor Moses (Nigeria & Chelsea) na mshindi wa mwaka 2015 Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon na klabu ya Borussia Dortmund.

Mgabon huyu alimaliza katika nafasi ya pili mwaka 2016 nyuma ya raia wa Algeria Riyad Mahrez, ambaye mwaka 2017 hakuingia katika orodha ya 30-bora.

Mkenya Victor Wanyama, ambaye pia alitajwa katika orodha ya 30-bora mwaka 2015 na 2016, hakufaulu kuingia katika orodha hii mwaka 2017.

Mshindi atatangazwa Desemba 11, 2017. 

 

Orodha ya kwanza ya wachezaji 30 (2017):

Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)

Bertrand Traore (Burkina Faso & Lyon)

Cedric Bakambu (DR Congo & Villarreal)

Christian Atsu (Ghana & Newcastle)

Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye)

Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

Eric Bailly (Ivory Coast & Manchester United)

Essam El Hadary (Misri & Al Taawoun)

Fabrice Ondoa (Cameroon & Sevilla)

Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco)

Jean Michel Seri (Ivory Coast & Nice)

Junior Kabananga (DR Congo & Astana)

Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord)

Keita Balde (Senegal & Monaco)

Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor)

Mbwana Samata (Tanzania & Genk)

Michael Olunga (Kenya & Girona)

Mohamed Salah (Misri & Liverpool)

Moussa Marega (Mali & Porto)

Naby Keita (Guinea & RB Leipzig)

Percy Tau (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns)

Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Dortmund)

Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

Thomas Partey (Ghana & Atletico Madrid)

Victor Moses (Nigeria & Chelsea)

Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto)

William Troost-Ekong (Nigeria & Bursaspor)

Yacine Brahimi (Algeria & Porto)

Youssef Msakni (Tunisia & Al Duhail)

Yves Bissouma (Mali & Lille)