Mkabaji Coquelin ayoyomea Valencia

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Thursday, January 11  2018 at  22:06

Kwa Mukhtasari

KIUNGO wa Arsenal, Francis Coquelin ataondoka uwanjani Emirates na kujiunga na klabu ya Valencia nchini Uhispania, kulingana na Kocha Arsene Wenger.

 

Kabla ya kipindi kifupi cha uhamisho kufunguka hapo Januari 1, tetesi zilienea kwamba Coquelin ataelekea katika Ligi Kuu ya Uhispania baada ya kuchezea Arsenal mechi moja pekee katika Ligi Kuu msimu huu.

Ripoti pia zilidai kwamba Mfaransa huyu mwenye umri wa miaka 26 alikuwa akimezewa mate na West Ham na Crystal Palace baada ya ufufuo wa Jack Wilshere katika klabu ya Arsenal kuzuia uwezekano wa Coquelin kupata namba kikosini.

Baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichotoka sare tasa dhidi ya Chelsea katika nusu-fainali ya shindano la League Cup hapo Jumatano, Wenger alithibitisha Coquelin atahamia nchini Uhispania.

Kwingineko, Uingereza itakabiliana na Nigeria uwanjani Wembley na Costa Rica uwanjani Elland Road katika mechi zake mbili za mwisho za kujipima nguvu mapema Juni kabla ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Na Mashirika