http://www.swahilihub.com/image/view/-/4759730/medRes/2109944/-/j8cbrnz/-/mwaki.jpg

 

Mwakinyo atua bungeni, ataka kuzichapa na Amir Khan

Bondia Hassan Mwakinyo akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kuwasili Bungeni  

Na THOMAS NG’ITU

Imepakiwa - Friday, September 14  2018 at  17:17

Kwa Muhtasari

Bondia huyo ameshinda pambano lake la TKO baada ya kumtandika mpinzani wake ngumi 96 katika raundi mbili

 

Dar es Salaam. Bondia Hassan Mwakinyo ametua Dar es Salaam alfajiri ya leo na kuungana na familia yake kwenda Bungeni Dodoma huku akiweka wazi lengo lake kwa sasa ni kuzichapa na Amir Khan.

Mwakinyo amerejea alfajiri (Ijumaa) kwa ndege ya Oman Air akitokea nchini England alipomchapa bondia wa Uingereza, Sam Eggington kwa TKO katika raundi ya pili kwenye pambano la raundi kumi lenye uzito wa Super Welter lililokuwa la utangulizi kabla ya kupanda Amir Khan aliyezichapana na Sam Vargas.

Akizungumza baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Mwakinyo alisema anamtamani kupambana na bondia Khan.

“Sisi wote ni watu unajua kwamba unaweza ukaona mtu jina lake lipo katika kiwango cha juu, lakini inakuwa tofauti na unavyokutana naye uwanjani, kwahiyo natamani nicheze hata na Khan,” alisema Mwakinyo.

Bondia huyo amewaomba Watanzania waendelee kumpa sapoti ili aendele kufanya mazoezi kwa juhudi ili kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.