Namimbia kumenyana na Kenya raga U20

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Friday, April 21  2017 at  06:40

Kwa Mukhtasari

MIAMBA Namibia watamenyana na Kenya katika fainali mashindano ya raga ya Afrika ya wanaume wasiozidi umri wa miaka 20 ya wachezaji 15 kila upande baada ya kupepeta wenyeji Madagascar 66-7 jijini Antananarivo, Alhamisi.

 

Chipu ya Kenya ilitangulia kufuzu baada ya kutoka chini 20-24 mapema katika kipindi cha pili na kushangaza Zimbabwe 34-24.  

Kenya itakuwa na mlima mkubwa wa kukwea katika fainali kwa sababu haijawahi kupiga mabingwa mara sita Namibia, ambao walishinda makala manne yaliyopita ya U/19 mara nne kabla ya mashindano haya kufanywa ya U/20 kuanzia mwaka 2017.

Mara ya mwisho Kenya na Namibia zilikutana katika fainali ilikuwa mwaka 2014. Kenya ilizabwa 52-17 jijini Windhoek.

Kabla ya Kenya na Namibia kuumiza nyasi katika fainali hapo Jumapili, Zimbabwe na Madagascar zitapigania medali ya shaba. Timu itakayopoteza mechi hiyo ya kutafuta nambari tatu itatemwa kutoka daraja hili la juu (A). Madagascar ilijaza nafasi ya Tunisia mwaka 2017 na huenda ikajipata imerejea daraja B mwisho wa makala haya.  

 

VIKOSI VYA KENYA NA NAMIBIA:

Kenya - Joshua Macharia, Derrick Keyoga, Victor Matiko, Benjamin Marshall, Stephen Keter, Henry Ayah, Mike Kimwele, Brian Ochieng, Toby Francombe, James Wanjala, William Diffu, Roxy Suchi, Mark Mutuku, Harold Anduvate, Gabriel Adero (nahodha), Melvin Thairu, Mike Munyua, Charles Tendwa, Steve Anthony, Xavier Kipng'etich, Edmund Anya, Jeff Mutuku, Stanley Isogol. Kocha – Paul Odera

 

Namibia - Andre Rademeyer, Obert Nortje, Sam Kuvare, Prince Gaoseb, Brandon Groenewald, Wihan von Wielligh, Rheinhardt Carelse, Chad Plato, Jay-C Olivier, Riaan de Klerk, Luke Jansen, Norman Erasmus, Nelius Theron, Jan Basson, Le Beau du Preez, Diamondo Tjombe, Marino Goagoseb, Tjingari Katjivi, Hans Niehaus, Alastair Miller, Collins Omalu, Rudi Pretorius, Romanzo Lento, Cliven Loubser, Lezardo Vos. Kocha - Roger Thompson