Okumbi aita wachezaji 28 kwa kambi ya Stars

Na JOHN ASHIHUNDU

Imepakiwa - Thursday, November 2  2017 at  15:07

Kwa Muhtasari

Kocha Stanley Okumbi amewaita kambini wanasoka 28 kuanza maandalizi ya kupambana na Zambia katika mechi ya kimataifa ya kupimana nguvu.

 

Mechi hiyo ya kirafiki itachezewa Kenyatta Stadium, Machakos mnamo Novemba 14.

Gor Mahia ambao majuzi walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu (KPL) wanaongoza kwa idadi ya wachezaji walioitwa baada ya jumla ya nyota wao saba kuitwa kwenye kikosi hicho cha Harambee Stars.

Walioitwa kutoka K’Ogalo wataongozwa na kipa Boniface Oluoch huku wengine wakiwa Wellington Ochieng’, Harun Shakava, Musa Mohammed, Ernest Wendo, Ken Muguna na George Odhiambo.

Vile vile Okumbi amewaita wachezaji kadhaa kutoka klabu za Supa Ligi ambao ni Bernard Ochieng’ na Chris Masinza kutoka Vihiga United, Simon Abuko wa KCB na Peter Ng’ang’a kutoka Nakuru All Stars.

Mshambuliaji Masoud Juma wa Kariobangi Sharks na Kepha Aswani wa Nakumatt pia wameitwa kwenye timu hiyo ya taifa.

Orodha ya makipa walioitwa ni: Boniface Oluoch (Gor Mahia), Gabriel Andika (AFC Leopards) na Patrick Matasi (Posta Rangers).

Walinzi ni: Benard Ochieng (Vihiga United), Wellington Ochieng (Gor Mahia), Dennis Sikhayi (AFC Leopards), Jockins Atudo (Posta Rangers), Harun Shakava (Gor Mahia), Musa Mohammed (Gor Mahia), Charles Momanyi (Kakamega Homeboyz) na Omar Mbongi (Ulinzi Stars).

Viungo ni: Ernest Wendo (Gor Mahia), Shaffan Siwa (Chemelil Sugar), Kenneth Muguna (Gor Mahia ), Patillah Omotto (Kariobangi Sharks), Peter Ng’ang’a (Nakuru All-Stars), Duncan Otieno (AFC Leopards), Chris Ochieng (Mathare United), Jackson Macharia (Tusker FC) na Whyvonne Isuzza (AFC Leopards).

Washambuliaji ni: Samuel Onyango (Ulinzi Stars), Kepha Aswani (Nakumatt), George Odhiambo (Gor Mahia), Masoud Juma (Kariobangi Sharks), Vincent Oburu (AFC Leopards) Chris Masinza (Vihiga United), Simon Abuko (KCB) na Ezekiel Otuoma (Western Stima).