Olunga kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika

Na JOHN ASHIHUNDU

Imepakiwa - Thursday, November 2  2017 at  15:09

Kwa Muhtasari

Mshambuliaji wa Harambee Stars, Micheal OIunga ni miongoni mwa wanasoka 30 watakaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka huu.

 

Straika huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa anaichezea klabu ya Girona ya Uhispania kwa mkopo yumo kwenye orodha ya watakaowania tuzo hiyo kwa kimombo kama “CAF African Player of the Year”. 

Olunga ni Mkenya wa pekee kwenye listi hiyo ambayo pia inamjumuisha Saidio Mane (Senegal na Liverpool), Mohammed Salah (Misri na Liverpool), Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns), Eric Bailly (Cote d’Ivorie na Manchester United) pamoja na Pierre Emerick Aubamayang ( Borussia Dortmund na Gabon), wote ambao wana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo. 

Kabla ya kuondoka nchini, Olunga alizichezea klabu za Liberty Sports Academy, Tusker, Thika United na Gor Mahia kati ya 2012 na 2015.