Kikosi cha KPL All Star kitakachopiga mechi za kirafiki Uhispania chatajwa

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, June 19   2017 at  08:30

Kwa Mukhtasari

KOCHA Stanley Okumbi ametaja wachezaji 20 kitakachozuru Uhispania mnamo Julai 17-25, 2017 kwa mechi mbili za kirafiki dhidi ya klabu za mbili zinazoshiriki La Liga.

 

Timu hiyo inayotakayofahamika kama KPL All Stars inajumuisha wanakabumbu 20 kutoka klabu za Ligi Kuu ya Kenya za Kariobangi Sharks, Tusker, Gor Mahia (watatu kila moja), AFC Leopards, Posta Rangers (wawili kila moja) nazo Thika United, Nzoia Sugar, Western Stima, SoNy Sugar, Sofapaka, Nakumatt na Ulinzi Stars zimechangia mchezaji mmoja kila moja.

Bandari, Kakamega Homeboyz, Chemelil Sugar, Zoo Kericho, Muhoroni Youth na Mathare United hazijafaulu kuwa na mchezaji katika kikosi hiki cha kwanza kitakachopunguzwa hadi 18 kabla ya safari hiyo ambayo La Liga imelipia kila kitu ikiwemo nauli ya ndege.

Okumbi, ambaye ananoa timu ya taifa ya Kenya ya watu wazima, atasaidiwa na John Kamau, ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Kenya wa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20.

Mpango wa Kenya kutuma wachezaji nchini Uhispania ni sehemu ya ushirikiano kati ya kampuni inayoendesha Ligi Kuu ya Kenya (KPL) na La Liga. Rais wa La Liga, Javier Tebas Medrano alikuwa nchini Kenya mwezi uliopita mnamo Mei 10-11.  

 

KIKOSI

Kipa – Farouk Shikalo (Posta Rangers), Mathias Kigonya (Sofapaka), Peter Odhiambo (Gor Mahia); Mabeki – Maurice Ojwang’ (Western Stima), Timothy Omwenga (Kariobangi Sharks), Robinson Kamura (AFC Leopards), Martin Kiiza (Tusker), Mohamed Musa (Gor Mahia);

Viungo - Ovella Ochieng’ (Kariobangi Sharks), Benson Iregi (Thika United), Boniface Muchiri (SoNy Sugar), Clinton Kisiavuki (Nakumatt), Patilah Omoto (Kariobangi Sharks), Jackson Macharia (Tusker), Simon Mbugua (Posta Rangers), Ernest Wendo (Gor Mahia), Humphrey Mieno (Tusker);

Washambuliaji – Victor Ogendo (Nzoia Sugar), Vincent Oburu (AFC Leopards), Samuel Onyango (Ulinzi Stars).