Paarwater abadilisha kikosi ili akomoe Urusi

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, November 13  2017 at  15:23

Kwa Muhtasari

BAADA ya kusikitishwa na kichapo kikali ambacho Kenya Simbas ilipata kutoka kwa Chile, Kocha Jerome Paarwater amefanya mabadiliko manane kabla ya kumenyana na Urusi hapo Novemba 14, 2017.

 

Simbas haikuwa na lake ilipozidiwa maarifa karibu katika kila idara iliponyukwa 23-3 katika mechi ya ufunguzi ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya Cup of Nations mnamo Novemba 10.

Shoka la Paarwater sasa limeangukia Moses Amusala, Curtis Lilako, George Nyambua, Nato Simiyu, Samson Onsomu, Tony Onyango, Jacob Ojee na David Ambunya walioanza dhidi ya Chile.

Nafasi zao katika kikosi kitakachoanza dhidi ya mabingwa watetezi Urusi zimetwaliwa na Vincent Mose, Peter Kilonzo, Alex Olaba, Biko Adema, Lyle Asiligwa, Oscar Simiyu, Dennis Karani na Martin Owilah. Olaba na Owilah hawakushiriki mechi ya Chile.

Urusi inaongoza jedwali kwa pamoja na Chile kwa alama nne. Ilizaba wenyeji Hong Kong 16-13 Novemba 10. Hong Kong ina pointi moja nayo Kenya inavuta mkia bila pointi. Kenya na Urusi hazijawahi kukutana katika raga ya wachezaji 15 kila upande.

Kenya inatumia shindano hili kujipiga msasa kabla ya Kombe la Afrika mwaka 2018 litakalotumika kuchagua mwakilishi wa Afrika katika Kombe la Dunia mwaka 2019.  

   

Kikosi cha Simbas kitakachomenyana na Urusi:

Wachezaji 15 wa kwanza

15. Vincent Mose, 14. Darwin Mukidza, 13. Peter Kilonzo, 12. Leo Owade, 11. Alex Olaba, 10. Biko Adema, 9. Lyle Asiligwa,1. Oscar Simiyu, 2. Peter Karia, 3. Dennis Karani, 4. Wilson K’Opondo (nahodha), 5. Oliver Mang'eni, 6. Davis Chenge,7. Martin Owilah, 8. Joshua Chisanga.

 

Wachezaji wa akiba

16. Philip Ikambili, 17. Moses Amusala, 18. Curtis Lilako, 19. George Nyambua, 20. Elkeans Musonye, 21. Samson Onsomu, 22. Nato Simiyu, 23. David Ambunya