http://www.swahilihub.com/image/view/-/5144236/medRes/2362969/-/12yuovuz/-/pamba+pic.jpg

 

Pamba , Geita zabanwa nyumbani

Na Saddam Sadick, Mwanza

Imepakiwa - Tuesday, June 4  2019 at  10:42

 

Mwanza.Timu za Pamba na Geita  zimeshindwa kutumia vyema viwanja vyao vya nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu katika mechi zao za kwanza za mchujo   jana.

Timu hizo za Ligi daraja la kwanza zinasaka nafasi ya kupanda kucheza Ligi kuu msimu ujao ili kuungana na Namungo na Polisi Tanzania ambazo zimekwishapanda.

Pamba ililazimishwa suluhu na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza huku Geita ikilazimishwa suluhu na Mwadui kwenye uwanja wa Geita.

Mwadui na Kagera Sugar zinapambana kubaki kubaki kucheza Ligi Kuu msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya 17 na 18 kwenye huku zikishuhudia African Lyon na Stand United zikishuka daraja moja kwa moja.

Kwenye uwanja wa Nyamagana Pamba ilishindwa kutumia uwanja wa nyumbani vyema ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kurudi kucheza Ligi Kuu baada ya kuikosa kwa miaka kadhaa tangu ilipoporomoka.

Pamba walitengeneza nafasi kadhaaa kupitia kwa Elias James na Shija Mkina lakini hawakuzitumia vema kuibuka na ushindi nyumbani.

Kagera Sugar nao watajilaumu kwa nafasi kadhaa walizopata kupitia kwa Peter Mwalyanzi dakika ya 44 na Ramadhan Kapera lakini walishindwa kuzitumia.

Timu hizo zitarudiana tena Jumamosi ambapo Kagera itakuwa nyumbani huku Mwadui pia ikicheza nyumbani mchezo wa marudiano utakaoamua timu itakayosalia Ligi Kuu msimu ujao.