Ratiba ya Ligi Kuu England hii hapa

Kombe la Dunia 

Imepakiwa - Thursday, June 14  2018 at  14:18

 

London, England. Mabingwa Manchester City wataanzia ugenini dhidi ya Arsenal katika ufunguzi wa Ligi Kuu England kati ya Agosti 11-12 katika ufunguzi wa Ligi Kuu England 2018-19.

Ratiba hiyo itakuwa ni kipimo sahihi kwa kocha Unai Emery aliyechukua jukumu la kuinoa Gunners.

Mechi nyingine za ufunguzi siku hiyo ni, Manchester United watakuwa wenyeji wa Leicester City, Liverpool itaonyeshana kazi na West Ham, mabingwa wa Ligi daraja la kwanza Wolverhampton Wanderers watakuwa nyumbani dhidi ya Everton kwenye Uwanja Molineux.

Timu nyingine zilizopanda daraja Fulham watakuwa wenyeji wa Crystal Palace, wakati Cardiff itakuwa ugenini dhidi ya Bournemouth.

Tottenham wataanza msimu ugenini dhidi ya Newcastle kwenye Uwanja wa St James' Park, wakati Chelsea itaivaa Huddersfield, Southampton dhidi ya Burnley, huku Watford watajiuliza kwa Brighton kwenye Uwanja wa Vicarage Road.

Ratiba ya ufunguzi

Arsenal v Manchester City

Bournemouth v Cardiff City

Fulham v Crystal Palace

Huddersfield Town v Chelsea

Liverpool v West Ham United

Manchester United v Leicester City

Newcastle United v Tottenham Hotspur

Southampton v Burnley

Watford v Brighton

Wolverhampton Wanderers v Everton