http://www.swahilihub.com/image/view/-/4802404/medRes/2138201/-/4of8w6z/-/reem.jpg

 

Real Madrid yamvalia njuga Sterling

Winga wa Manchester City, Raheem Sterling  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, October 12  2018 at  09:21

Kwa Muhtasari

Amebakiza miezi 18 kabla ya mkataba kumalizika akiwa analipwa mshahara wa Pauni180, 000 kwa wiki


 

Madrid, Hispania. Real Madrid imekosa utulivu kuhusu winga wa Manchester City, Raheem Sterling ambaye amekuwa katika kiwango bora.

Real Madrid imerusha ndoano kwa mara nyingine kwa nyota huyo wa kimataifa wa England, ikitaka saini yake katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwakani.

Sterling amekuwa kwenye ubora tangu alipotua kocha Pep Guardiola ambaye amekuwa akimtumia katika kikosi cha kwanza.

Pia Real Madrid inataka kujiimarisha kwa kumsajili nyota wa Chelsea Eden Hazard ingawa inakabiliwa na kibarua kigumu kupata saini yake Januari.

Klabu hiyo inataka kujenga timu imara, baada ya Zinedine Zidane kuondoka ghafla licha ya kuipa mafanikio katika mashindano ya Ulaya.

Taarifa Hispania zimedai Sterling ndiye chaguo la kwanza kwa Real Madrid kulinganisha na wachezaji wengine wa Ulaya.

Sterling amebakiza miezi 18 kabla ya mkataba kumalizika akiwa analipwa mshahara wa Pauni180, 000 kwa wiki na bado hawajakubaliana kuhusu mkataba mpya.

Kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui amevutiwa na kiwango cha nyota huyo wa zamani wa Liverpool mwenye kasi uwanjani.

Katika mechi 47 alizocheza msimu uliopita, Sterling amefunga mabao 23 katika kikosi cha Man City.