http://www.swahilihub.com/image/view/-/4842130/medRes/2163990/-/q702shz/-/canavaro.jpg

 

Shughuli ya Cannavaro yapigwa ‘stop’

Aliyekuwa nahodha wa timu Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’  

Na BERTHA ISMAIL

Imepakiwa - Thursday, November 8  2018 at  10:52

Kwa Muhtasari

Niwaombe wajumbe ajenda hii iishie hapa na tuitoe kwenye ajenda za mpango mkakati

 

Arusha. Uongozi wa Yanga imewapiga ‘stop’ wanachama wa tawi la Arusha kufanya sherehe ya kumuaga aliyekuwa nahodha wa timu yao kwa zaidi ya miaka 10 Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Baada ya Cannavaro kutangaza kustaafu soka, uongozi wa Yanga uliandaa mechi mbili maalumu kwa ajili ya kumuaga kabla ya kumpatia nafasi ya Umeneje.

Wanachama wa Yanga tawi la Arusha nao walikuwa na lengo la kumuaga Cannavaro kwa kucheza mechi lakini kabla ya kufika mbali walipowasiliana na uongozi wa juu walikataa.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu Katibu Mkuu wa tawi hilo, Destrich Kateule alisema katika ajenda za mkutano uliopita za maandalizi ya sherehe ya kumuaga Cannavaro imefikia tamati na kuisitisha.

“Tulikuwa tumefikia pazuri kwenye maandalizi ya sherehe yetu lakini niwaombe wajumbe ajenda hii iishie hapa na tuitoe kwenye ajenda za mpango mkakati ingawa tumefikia pazuri, uongozi wa Yanga Makao Makuu wamesema hawatutambui maana tawi letu limekufa,” alisema Kateule.

Kateule alisema majibu hayo aliyopewa na katibu wa matawi ya Yanga yameenda sambamba na kuwataka kufanya Uchaguzi Mkuu ikiwa ni pamoja na kuorodhesha wanachama zaidi ya 100 jambo ambalo wanatakiwa kulifanya kwasasa.

“Kama mlivyotutuma tulienda na ajenda zile ikiwemo kuileta timu Arusha ili wadau wawaone wachezaji wa sasa kama Morogoro walivyofanya ili tumuage mwenzetu lakini tuliambiwa hatuna hadhi ya kukabidhiwa timu, tufanye uchaguzi kwanza ,”

Kufuatia hali hiyo wanachama kwa pamoja waliazimia Jumapili ya Novemba 11 wakutane kwa ajili ya zoezi la kujiandikisha ambapo sasa tawi hilo lina zaidi ya wanachama 30 ili wafikie wanachama 100 ndipo wafanye uchaguzi mkuu kama walivyoelekezwa.