http://www.swahilihub.com/image/view/-/5128022/medRes/1626073/-/urfttr/-/simbu+pic.jpg

 

Simbu kupeleka makali Marekani

Na Eliya Solomon

Imepakiwa - Thursday, May 23  2019 at  11:43

 

Arusha. Wanariadha watano WA Tanzania wanatarajia kushiriki mbio za "Boulder to Boulder 10k" zitakazofanyika Jimbo la Colorado, Marekani Mei 27, mwaka huu.

Mashindano hayo ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka katika mji wa Boulder, wanariadha nyota kutoka Tanzania wanatarajia kuondoka Leo jioni alhamis kuelekea nchini humo kuungana na wanariadha wengine kutoka mataifa mbali mbali.

Ofisa habari wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Tullo Chambo  amewataja wanariadha hao kuwa ni Alfonce Simbu, Gabriel Geay, Josepha Panga ambao wataongozana na wasichana wawili Magdalena Shauri na Natalia Elisante.

Geay amesema kuwa ana matumaini ya kushinda mbio hizo kutokana na kuzifahamu vema barabara yake lakini pia amekwisha zoea mazingira.

Geay alisema kuwa maandalizi ya mbio hizo amefanya tangu mwezi March kutokana na tiyari alishapata ratiba hivyo ana uhakika wa kutetea medali yake ya dhahabu aliyoitwaa mwaka jana.

Kwa upande Simbu amesema kuwa anakwenda kushiriki akijua macho mengi ya watanzania yanamtazama yeye hivyo atakimbia kizalendo kuhakikisha anairejesha heshima yake katika mbio kama kipindi cha nyuma

 (Bertha Ismail)

DTB yapania makubwa SDL

Dar es Salaam. Baada ya kufuzu Ligi Daraja la Pili, kocha wa DTB, Michael Lugalela, amesema umoja ndio nguzo pekee iliyowafanya kufikia malengo yao.

“Ligi ya mabingwa wa mikoa tumevuka salama, pongezi za dhati ziende kwa wachezaji, viongozi wetu wa juu ambao siku zote wamekuwa wakituunga mkono pamoja na mashabiki zetu, tumeshirikiana,” alisema Kocha huyo.

Lugalela  ambaye ni kocha mchezaji, alisema ili kikosi chake kuendana na kasi ya ushindani ya daraja la pili atakiboresha kwenye baadhi ya maeneo muhimu.

Fainali ya Ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL) ilichezwa mkoani Simiyu ilikutanisha timu nane zilizopangwa katika makundi mawili. Kundi A, lilikuwa na timu za DTB, Isanga Rangers, Top Boys na Bariadi United.

Baada ya michezo ya makundi, timu tatu zilifanikiwa kufuzu kucheza Ligi daraja la  pili ngazi ya taifa, ikiwemo DTB kwa msimu wa 2019/20 huku nyingine zikiwa Pan African na Mbuni FC  kutoka Arusha.