Viwango vya Raga: Kenya yashuka

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, November 20  2017 at  17:24

Kwa Muhtasari

KENYA inazidi kupoteza umaarufu katika raga ya wachezaji 15 ya wanaume baada ya kutupwa nafasi moja chini hadi 30 katika viwango bora vipya vilivyotangazwa Jumatatu.

 

Mabingwa hawa wa Afrika mwaka 2011 na 2013 waliteremka katika msimamo huo wa mataifa 103 baada ya kulimwa 40-30 na Hong Kong katika Kombe la Mataifa mnamo Novemba 18, 2017. Ilianza mashindano haya ikiwa katika nafasi ya 27.

Imeshuka hadi nafasi ya 30 baada ya pia kupepetwa na Urusi 31-10 na kupapurwa 40-30 na Hong Kong.

Mabingwa mara saba wa Afrika, Namibia, pia wameteremka kwenye viwango hivi. Walinyukwa 52-36 na Uruguay jijini Windhoek.  

 

Afrika (10-bora):

1. Afrika Kusini (imesalia nafasi ya tano duniani)

2. Namibia (imeteremka nafasi mbili hadi 23 duniani)

3. Kenya (imeshuka nafasi moja hadi 30 duniani)

4. Uganda (imebaki nafasi ya 35 duniani)

5. Tunisia (imepaa kutoka nafasi ya 41 hado 40 duniani)

6. Morocco (imekwamilia nafasi ya 44 duniani)

7. Zimbabwe (imesalia nafasi ya 46 duniani)

8. Madagascar (haijasonga kutoka nafasi ya 48 duniani)

9. Senegal (imebaki nafasi nafasi ya 50 duniani)

10. Ivory Coast (imesalia katika nafasi ya 51 duniani)

 

Duniani (30-bora):

1. New Zealand

2. Uingereza

3. Australia

4. Ireland

5. Afrika Kusini

6. Scotland

7. Wales

8. Ufaransa

9. Argentina (imepaa nafasi moja)

10. Fiji (imeshuka nafasi moja)

11. Japan

12. Georgia

13. Italia

14. Romania (iko juu nafasi moja)

15. Tonga (imeteremka nafasi moja)

16. Samoa

17. Marekani

18. Uruguay (imeruka juu nafasi moja)

19. Urusi (imeshuka nafasi moja)

20. Uhispania

21. Canada (imeimarika nafasi mbili)

22. Namibia (iko chini nafasi moja)

23. Hong Kong (imepaa nafasi moja)

24. Ujerumani (imeshuka nafasi mbili)

25. Ureno

26. Uholanzi (imepanda nafasi mbili)

27. Brazil (imeruka juu nafasi tatu)

28. Chile (imeteremka nafasi moja)

29. Ubelgiji (imetupwa chini nafasi tatu)

30. Kenya (imeshuka nafasi moja)