Wakenya wafagia nafasi 5 za kwanza Athens Marathon

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Sunday, November 12  2017 at  14:50

Kwa Muhtasari

SAMUEL Kalalei ameongoza Wakenya kufagia nafasi tano za kwanza katika kitengo cha wanaume cha mbio za Athens Marathon nchini Ugiriki, Jumapili. 

 

Kalalei aliacha kabisa mpinzani wake wa karibu Milton Rotich aliyepigiwa upatu kutwaa ubingwa baada ya kilomita 35. Alinyakua taji kwa saa 2:12:17, huku Rotich akiridhika katika nafasi ya pili (2:14:18) naye Jonathan Yego akafunga tatu-bora (2:16:08). 

Kitengo cha wanawake kilishuhudia ushindani mkali zaidi, huku Muethiopia Bedaru Badane akikata utepe kwa saa 2:34:18, sekunde nne mbele ya Mkenya Alice Jepkemboi. Malkia wa mwaka 2016, Nancy Arusei, pia kutoka Kenya, alimaliza wa tatu kwa saa 2:34:51. Wakimbiaji 18, 500 kutoka mataifa 100 walishiriki makala ya mwaka huu.

 

Matokeo ya Athens Marathon (Novemba 12):

Wanaume

Samuel Kalalei (Kenya) saa 2:12:17

Milton Rotich (Kenya) 2:14:18

Jonathan Yego (Kenya) 2:16:08

John Komen (Kenya) 2:16:26

Evans Biwott (Kenya) 2:16:36

 

Wanawake

Bedaru Badane (Ethiopia) saa 2:34:18

Alice Jepkemboi (Kenya) 2:34:22

Nancy Arusei (Kenya) 2:34:51.