Wanasukari nguvu sawa

Na CHRIS ADUNGO

Imepakiwa - Tuesday, October 24  2017 at  21:18

Kwa Muhtasari

CHEMELIL Sugar walizimishiwa sare ya 2-2 mbele ya mashabiki wao wa nyumbani mnamo Oktoba 24, 2017 katika mechi ya Ligi Kuu ya KPL iliyowakutanisha na mabingwa wa 2006, SoNy Sugar uwanjani Chemelil Complex.

 

Chemelil kwa sasa wanasalia katika nafasi ya tisa kwa alama 37, moja zaidi kuliko SoNy ambao wanajivunia idadi sawa ya pointi na Bandari na mabingwa mara 13 wa KPL, AFC Leopards.

Nyota George Abege aliwafungulia SoNy Sugar ukurasa wa mabao kunako dakika ya 14. Amani Kyata aliwarejesha Chemelil mchezoni kwa kufungwa mkwaju wa penelti baada ya fowadi Collins Netto kuchezewa visivyo mwishoni mwa dakika ya 27.

Benjamin Mosha aliwafungia SoNy Sugar bao la pili kunako dakika ya 64 baada ya kukamilisha kwa ustadi krosi ya Abege lakini Philip Muchuma akasawazisha mambo katika dakika ya 72 baada ya kushirikiana vilivyo na kiungo John Mwita.

SoNy kwa sasa wanajiandaa kuvaana na Nakumatt, Thika, Sofapaka, Gor Mahia na Muhoroni Youth kwa usanjari huo. Kwa upande mwingine, Chemelil wanakabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya AFC Leopards.

Tusker, Kakamega Homeboyz na Western Stima katika jumla ya michuano minne ijayo.