Wanyama kushiriki mechi dhidi ya Bournemouth

Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Monday, October 9  2017 at  17:21

Kwa Muhtasari

NAHODHA wa Harambee Stars, Victor Wanyama anatarajiwa kurejea kuchezea klabu yake ya Tottenham Hotspur mnamo Oktoba 14, 2017 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza.

 

Habari kutoka kambi ya Spurs inasema Wanyama, ambaye amekuwa akiuguza jeraha la goti tangu Agosti 20, 2017, anatarajiwa kushiriki mechi ya Bournemouth uwanjani Wembley.

Kiungo huyu Mkenya alijiondoa kwa ziara ya Stars nchini Iraq na Thailand kwa sababu ya jeraha hilo. Kenya ililimwa 2-1 na Iraq na kupoteza 1-0 dhidi ya Thailand.

Kiungo Mousa Dembele kutoka Ubelgiji pia anatarajiwa kurejea katika kikosi cha Spurs hapo Oktoba 14. Amekuwa mkekani na jeraha la kifundo.

Spurs inashikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la Ligi Kuu kwa alama 14 kutoka mechi saba. Bournemouth iko katika nafasi ya 19 kwa alama nne.