http://www.swahilihub.com/image/view/-/5113842/medRes/2342427/-/xw49ag/-/krikate+pic.jpg

 

Watanzania watakata karate Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Imepakiwa - Tuesday, May 14  2019 at  09:37

 

Dar es Salaam.  Wachezaji karate wa Tanzania, Mikidadi Kilindo na Elisiana Katani wameibuka washindi wa mashindano ya kata kwa upande wa wanaume na wanawake katika mashindano ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyomalizika jijini Kampala, nchini Uganda hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la JKA Tanzania, Fedeliko Nestory amewasifu wachezaji hao kwa kushinda medal hizo, sio kwa wao binafsi, bali kwa nchi pia.

Kilindo, mwenye dani 4 ( maarufu Ganchan) ambaye pia ni Mkufunzi Mkuu msaidizi wa JKA/Tanzania, ameshinda medali ya dhahabu, baada ya kuwashinda washiriki wengine kutoka nchi zaidi ya 10 zilizoshiriki katika upande wa kata (kuonyesha maarifa ya kupigana) kwa upande wa wanaume. Hii ni mara ya tano kwa Ganchan kushinda taji hili.

Pia ni mara ya kwanza kwa kushinda taji hili, akiwa miongoni mwa wanawake wachache wanaocheza mchezo huu hapa nchini.

Katani, ambaye pia ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utoaji taarifa kwa Umma wa JKA/World Federation-Tanzania, ameshinda medali ya fedha , baada ya kushinda nafasi ya pili katika upande wa wanawake.

 “Tunashukuru Mungu tumeshinda medali, tunaomba wadau wasaidie kuukuza mchezo huu hapa nchini,” wamesema Kilindo na Katani kutokea Kampala, kupitia ukurasa wa Facebook wa JKA/WorldFederation-Tanzania.

Nestory amesema wawakilishi hao wameipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa, huku akiomba serikali, mashirika ya umma, makampuni na watu binafsi kusaidia katika ukuaji na ushiriki wa mchezo huo katika michuano ya kimataifa.

“Tuna mashindano mengi katika kalenda yetu yam waka, hivyo tunaomba wadau watusaidie,”

Amesema kuanzia July 1-7, Tanzania itakuwa mwenyeji wa semina ya ya Gasshuku na Mashindano ya kimataifa ambapo nchi 15, ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Angola, Botswana, Madagascar, Zimbabwe, Jamhuri ya Kongo na Afrika ya Kusini zimethibitisha ushiriki.