http://www.swahilihub.com/image/view/-/1660216/medRes/431073/-/adyl2mz/-/Mututho.jpg

 

Hisia kali Mututho kumteua mwalimu wa kike, 26 mgombea mwenza

John Mututho

Bw John Mututho akihutubu awali. Picha/MAKTABA 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Sunday, January 1  2017 at  14:55

Kwa Mukhtasari

ALIYEKUWA mbunge wa Naivasha John Mututho amemteua mwalimu wa sekondari mwenye umri wa miaka 26 kuwa mgombea mwenza wa kiti cha Ugavana wa Nakuru.

 

Uteuzi wa Bi Maurine Chebet umezua hisia mbali mbali kutoka eneo hilo huku akipongezwa kwa uamuzi wake.
Wakazi wa Kaptembwa, Mauche, Kuresoi na Rongai katika kaunti ya Nakuru wameunga mkono uamuzi wa Bw Mututho.

Bi Chebet atakuwa kiongozi mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuingia katika uongozi wa kaunti.

“Mututho ameweka historia kwa kumtambua mwanamke mwenye umri mdogo kutoka eneo la Kapkores eneo la Kuresoi kusini kuwa mgombea mwenza. Hii ni ishara kwamba anatambua watu waliosahaulika ,” alisema Bw John Mungai.

Bi Janet Chumo, ambaye ni mwakilishi wa kina mama bungeni kutoka Kuresoi, alisema chaguo la Bw Mututho lafaa kwa vile anatambua jinsia na wanarika.

Bi Chumo alisema atawaunga mkono Bw Mututho na Bi Chebet wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Kaunti ya Nakuru iko na rasilmali nyingi lakini kwa sababu ya uongozi mbaya haijastawi. Kuikomboa Bw Mututho ndiye dawa,” aliiongeza kusema..

Bw Robert Too, ambaye ni mkazi wa Kuresoi kusini, alisema kati ya Sh44 bilioni ambazo Gavana Kinuthia Mbugua alipokea kutoka kwa Serikali kuu ni mradi mmoja tu wa Mochari ambao ulizinduliwa katika hospitali ya wilaya ya Olenguruone.