http://www.swahilihub.com/image/view/-/3288086/medRes/1376272/-/gbo3ad/-/NAMWAMBA.jpg

 

Namwamba: Kuitwa fuko wa Jubilee kulinisukuma kuhama ODM

Ababu Namwamba

Aliyekuwa mbunge wa Budalang'i Ababu Namwamba ahutubia wafuasi awali. Picha | TONNY OMONDI  

Na LEONARD ONYANGO

Imepakiwa - Thursday, January 5   2017 at  12:04

Kwa Mukhtasari

MBUNGE wa Budalangi Ababu Namwamba sasa anasema kubandikwa 'kibaraka wa Jubilee’ kulimkera mno kiasi cha kufanya uamuzi 'mgumu’ wa kugura chama cha ODM.

 

Bw Namwamba aliyekuwa akizungumza kwenye mahojiano na runinga ya Citizen alichafuliwa nyongo mno na madai hayo yaliyomhusisha na serikali ya Jubilee licha ya kuwa Katibu Mkuu wa ODM.

Bw Namwamba ambaye sasa ni kiongozi wa chama cha Labour Party of Kenya (LPK) alisema, aliomba ushauri kutoka kwa kinara wa ODM Raila Odinga kuhusiana na hatua aliyopaswa kuichukua baada ya kuchipuka kwa madai hayo.

“Ilikuwa mara ya kwanza kusikia neno 'kibaraka’ na nilipigwa na butwaa niliposikia nikirejelewa kuwa 'kibaraka wa Jubilee ndani ya ODM’,” akasema Bw Namwamba.

Alisema aliomba ushauri kutoka kwa Bw Odinga kwa sababu madai hayo yalikuwa yakitolewa na wandani wake wa karibu.

“Nilikuwa nasikia madai hayo kutoka kwa Oburu Odinga, ambaye ni nduguye Raila, Eliud Owala , meneja wa kampeni za Bw Odinga.

“Hapo ndipo niliuliza Bw Odinga ikiwa madai hayo yalikuwa yakitolewa kwa niaba yake. Kadhalika, niliuliza Bw Odinga ikiwa kulikuwa na tatizo mimi kuendesha shughuli za chama katika wadhifa wa katibu mkuu. Lakini alinijibu kwamba hakukuwa na tatizo,” akasema Bw Odinga.

Bw Namwamba alisisitiza kuwa uhusiano baina yake na viongozi wa Jubilee ulikuwa wa kimaendeleo.

Mbunge huyo pia alidai kuwa alipokea taarifa za kijasusi kuwa baadhi ya vijana walipanga kusambaratisha uchaguzi wa viongozi wa ODM uwanjani Kasarni mnamo Februari 2014 ambapo alikuwa akiwania wadhifa wa katibu mkuu.