Gavana adai wendawazimu kisiasa wameingia Murang'a

Gavana wa Murang’a

Gavana wa Murang'a Mwangi wa Iria. Picha/MAKTABA 

Na MWANGI MUIRURI

Imepakiwa - Saturday, January 7  2017 at  17:29

Kwa Mukhtasari

Gavana wa Murang’a Bw Mwangi wa Iria amedai kuwa 'soko la siasa Murang’a limejazana wendawazimu ambao wanachokora mapipa ya propaganda dhidi ya utawala wake'.

 

GAVANA wa Murang’a Bw Mwangi wa Iria amedai kuwa 'soko la siasa Murang’a limejazana wendawazimu ambao wanachokora mapipa ya propaganda dhidi ya utawala wake'.

Akijibu mipigo ya mbunge wa Kigumo Bw Jamleck Kamau ambaye asubuhi alizindua kampeni zake rasmi za kumfurusha Bw wa Iria mamlakani 2017,
Bw Wa Iria alisema kuwa “huyu sio mchezaji wa ligi yangu kwa kuwa yake ni ile ya limbukeni yangu ikiwa ya waliokomaa.”

Alisema kuwa sawa na vile kila soko halikosi wa akili taahira, soko la kisiasa Murang’a limejidhihirisha kuwa na wake wa upungufu uo huo.

Akasema: “Mnawajua. Leo nimeona wameingia katika maeneo kadha ya kaunti hii wakisema kuwa hakuna lililofanywa na serikali yangu.
Wanapitia kwa wachuuzi ambao nimewajengea vibanda na nitawapunguzia ada za ushuru wakisema kuwa sijafanya kazi.”

Alisema kuwa kuna wakati mmoja msafara wa “mmoja wa hao wendawazimu” ulisimama katika jokovu la maziwa mjini Sabasaba na ambao ni mradi wa
serikali ya kaunti wa kuwafaa wafugaji maziwa kuhifadhi bidhaa hiyo ikingoja soko.”

Akasema: “Akiwa kando mwa jokovu hilo ambalo ni moja ya zingine 35 kote Murang’a, alisema kuwa hatujafanya kazi. Akasema kuwa kazi yetu ni ufisadi na kujipiga kifua huku tukijigamba. Hawa ni watu wa kuhurumiwa kisiasa.”

Alisema kuwa “siku hizi raia wamepevuka macho kiasi kwamba ukiwaomba kura zao kupitia njia za uongo watakucheka tu na hatimaye uishie
kujuta baadaye wakikuangusha. Mimi kama wa Iria najua yangu ambayo nimeyatekeleza katika kipindi cha utawala wangu wa awamu moja tu yananitetea pakubwa. Wacha wasio na kazi warandarande mitaani.”

Kuhepa majukumu

Bw wa Iria aliteta kuwa kuna wanasiasa ambao wamehepa majukumu yao ya kuchaguliwa na ambapo kwa sasa wamejitwika majukumu mengine ya kuwa
sumbua.

“Mtu alichaguliwa kuwa mbunge wa Kigumo kwa miaka mitano. Mwaka mmoja kabla ya majukumu hayo kukamilika, ashawahepa waliomchagua na kwa sasa anarandaranda kote katika kaunti akisema akumbatiwe kama kiongozi. Utahepa je majukumu yako rahisi ukimbie kuomba majukumu mengine
magumu?" akahoji.